Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza NMB Bank kwa kuanzisha Programu mbali mbali walizozilenga kwa kuwanufaisha Wananchi.

Rais Dkt. Mwinyi ameeleza hayo kupitia Hotuba iliyosomwa kwa Niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hmed Suleiman Abdulla katika wa uzinduzi wa Jukwaa la Go na NMB uliofanyika katika Viwanja vya Bustani ya Forodhani Jijini Zanzibar.

Ameeleza kuwa hatua iliyochukuliwa na Bank hiyo ya kuanzisha Jukwaa hilo linalolenga kutoa mikopo na vitendea kazi ambapo Vijana wataweza kujiajiri kupitia Uvuvi, Boda boda na Mama lishe hatua ambayo itasaidia kutatua changamoto za kupata mitaji zinazokwamisha Malengo ya Wananchi kujiajiri.

Sambamba na hayo Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kwa dhati kuboresha na kuendeleza elimu ya fedha katika ngazi zote ili kuwajengea Wananchi uelewa juu ya masuala ya kibenki.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa fursa zilizopo katika Jukwaa hilo zitasaidia kuondosha tabia ya baadhi ya Kampuni zenye kujipatia kipato kupitia nguvu za Wananchi kwa kutumia mwanya wa kukopesha na hatimae kuwatapeli Wananchi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna ameeleza kuwa lengo la kuanzisha Programu hiyo ya Go na NMB ni kuwaweka karibu vijana katika Jukwaa moja kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Nane katika kukuza Uchumi wa Nchi.

Aidha ameeleza kuwa zaidi ya Asilimia Sitini ya Watanzania ni Vijana jambo ambalo limepelekea NMB kuelekeza nguvu hizo kwao kwa kuzalisha ajira na kusaidia kujikwamua kiuchumi.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe. Rashid Simai Msaraka ameeleza kuwa NMB imeonesha kuunga Mkono Azma ya Serikali kukaribisha Taasisi Binafsi kuungana na Serikali katika kuwaletea maendeleo Wananchi wake.

Aidha Mhe. Msaraka ameeleza kuwa Jukwaa hilo litawasaidia Kina Mama na Vijana kujipatia Mikopo nafuu itakayowasaidia kujipatia kipato na kujikwamua kimaisha na kuisaidia Serikali katika kuwawezesha wananchi wake.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Sueiman Abdulla akimkabidhi Hundi ya Shilingi za kitanzania Milioni mbili (2,000,000/=) Mshindi wa Kwanza wa mbio za Ngalawa bwana Omari Haji Haji mashindano yaliyodhaminiwa na NMB
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akitoa nasaha zake katika uzinduzi wa Jukwaa la Go na NMB uliofanyika katika Viwanja vya Bustani ya Forodhani Zanzibar ambapo aliipongeza Benki hiyo kuanzisha Jukwaa hilo litakalowasaidia Wananchi kujikwamua kiuchumi kwa kupata mikopo nafuu inayotolewa na Benki hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...