- Atoa zaidi ya shilingi Bilioni 21 za Ujenzi wa kilomita 14 Za barabara, mitaro zinajengwa Na wakandarasi watatu.


- Wananchi wafurahishwa kuona kero ya mafuriko kila mwaka imepata ufumbuzi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametembelea Ujenzi wa Barabara, Taa, Mitaro, Mifereji ya maji Kata ya Mbweni zenye urefu wa Km 14.5 inayogharimu Zaidi ya Shilingi Bilioni 21 ambapo kukamilika kwake inakwenda kilio Cha muda mrefu Cha Wakazi wa Mbweni.

Akizungumza wakati wa Ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo, RC Makalla amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha zaidi ya Shilingi Bilioni 21 kwaajili ya Kata ya Mbweni Baada ya kupokea Kilio Cha Wakazi hao.

Miongoni mwa Barabara alizotembelea RC Makalla ni pamoja na Barabara ya Mbweni JKT yenye urefu wa Km 3.9 inayojengwa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Nyanza road works kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.5 na Sasa Ujenzi upo Asilimia 50.

Aidha RC Makalla ametembelea Ujenzi wa Barabara ya Mkwajuni Mbweni yenye urefu wa Km 7 Chini ya Mkandarasi kutoka Kampuni ya Kings Building kwa gharama ya Shilingi Bilioni 11.2 ambapo Ujenzi umefikia Asilimia 72.

Hata hivyo RC Makalla amekagua Ujenzi wa Barabara ya Mbweni kwa Somji yenye urefu wa Km 2.1 ambapo ametumia ziara hiyo kutoa wito kwa Wakandarasi kumaliza kazi kwa wakati ili waweze kujiwekea mazingira ya kupata kazi Mara kwa mara.

Pamoja na hayo RC Makalla amempongeza Rais Samia kwa kutoa Shilingi Bilioni 9 kwaajili ya Ujenzi wa Mifereji ya maji kwenye maeneo yaliyokuwa yakikabiliwa na tatizo la mafuriko na maji kutwama kwenye Kata hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...