Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comredi Juma Homera ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo
Tanzania (TARI) kwa kuandaa maonesho ya kilimo biashara katika mashamba ya mfano ya
TARI Uyole kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo likiwemo Baraza la Nafaka la
Afrika Mashariki (EAGC).
Katika hotuba yake wakati akifungua maonesho hayo, Comrade Homera amewataka wakulima
na wadau wa kilimo kuzingatia kanuni bora za kilimo kwa kutumia mbegu bora na kushirikiana
na wataalam wa kilimo ili kupata utaalam wa uzalishaji wa mazao yenye tija katika kuinua
uchumi wa nchi.
Aidha, amezitaka Taasisi za huduma za kilimo zikiwemo Wakala wa pembejeo (mbolea, mbegu
bora na viuatilifu) kuweka programu endelevu za upatikanaji wa pembejeo hizo na kuwataka
wataalam wa kilimo kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbegu bora, mbolea na
viuatilifu kwa wakulima ili .kuongezea tija.
Maonesho hayo yaliyobeba kaulimbiu inayosemayo "Mageuzi ya Kilimo Biashara, Jiandae
Kuhesabiwa kwa Mipango Endelevu" ni sehemu ya utekelezaji wa Agenda 10/30
inayoongozwa na kaulimbiu ya Kilimo Biashara.
Akitoa salami za TARI katika maonesho hayo, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Dkt. Richard
Kasuga, alimshukuru mgeni rasmi na uongozi wa mkoa wa Mbeya kwa kuweka kipaumbele
kusaidia Utafiti hususan Kituo cha TARI Uyole.
Aidha, Dkt. Kasuga ameipongeza na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na
Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Kilimo
chini ya Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe kwa kutenga fedha kwa ajili ya utafiti na
kuzalisha mbegu bora ili kuongeza tija, kuwa na uhakika wa chakula, kipato, kuboresha lishe na
kuchangia ukuaji wa uchumi katika nchi.
Dkt. Kasuga ameongeza kuwa katika mwaka 2021/22 Serikali iliitengea TARI shilingi bilioni 11
kwa ajili ya fedha za maendeleo kutoka takribani Shilingi bilioni 7 mwaka 2020/21, na katika
mwaka 2022/23 Serikali imeitengea TARI Shilingi bilioni 41 fedha za maendeleo ambazo .
zitachangia ufikiwaji wa Agenda 10/30 kwa kuongeza upatikanaji wa mbegu bora na
kuendeleza utafiti wa kilimo nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha TARI Uyole Dkt. Tulole L. Bucheyeki amesema
maonesho haya ya Kilimo Biashara ambayo yanafanyika kwa mwaka wa nne (4) mfululizo,
yameonyesha mafanikio makubwa kwa kuwaunganisha wadau wa kilimo katika mnyororo wa
thamani.
Dkt. Bucheyeki ameongeza kuwa, matokeo ya utafiti hayawezi kuleta tija inayokusudiwa bila
kushirikisha wadau wa kilimo katika kuzisambaza teknolojia hizo ili zilete matokeo tarajiwa..
Katika maonesho ya kilimo biashara, TARI ilitambulisha teknolojia za mazao ya nafaka (ngano,
mahindi na ulezi), maharage, soya pareto, viazi mviringo, parachichi na uhandisi kilimo.
Taasisi na makampuni mengine yaliyoshiriki maonesho ya kilimo biashara ni Seed Co, Kibo
Seed, Highland Seed Growers, Beula Seed, Agriseed, Mashamba and Tractor, Syngenta
Tanzania, Agro Z, na Mosanto. Mengine ni YARA, Minjingu, Zam seed, Meru Agro, CORTEVA,
MATI Uyole, TALIRI, Western Seed na PANNAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...