KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amewataka wakuu wa mikoa kote nchini wenye wakulima wa korosho kuacha urasimu na kuharakisha usambazaji na ugawaji wa pembejeo kwa wakulima hao.
Komredi Shaka ametoa maagizo hayo baada ya kusikia malalamiko ya wananchi katika kijiji cha Lukuledi mwanzoni kwa ziara yake ya siku nne mkoani Mtwara. Wananchi hao walilalamikia kuchelewa kupewa pembejio za zao la Korosho.
“Hili nalisema kwa wakuu wote wa mikoa wenye wakulima wa korosho waondoe urasimu na wagawe haraka pembejeo hizi, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa naomba kamati zako ziharakishe ugawaji wa pembejio hizi” alisema Shaka
Amesema serikali ya CCM awamu ya sita inayongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeamua kugawa pembejeo bure kwa wakulima hivyo kuzichelewesha ni kufifisha nia nzuri ya serikali ya kuwapunguzia gharama wakulima na kuongeza tija kwao.
"Asubuhi Mkuu wa Mkoa alinipa taarifa kwamba pembejeo zimeshafika tangu tarehe 18 Mei, 2022 kwa hivyo niwatake Serikali ya Mkoa wa Mtwara waache urasimu, ndani ya wiki moja pembejeo ziwe zimetoka na kuwafikia wakulima. Tunataka wananchi wanufaike na hatua ya Rais Samia ambaye ameamua kutoa pembejeo bure kwa lengo kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao." Amesema Shaka.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Meja Jenerali Marko Gaguti, amesema amepokea maelekezo hayo na anayafanyia kazi kabla ya siku saba zilizotolewa na Chama kupitia kwa katibu wa NEC itikadi na uenezi Ndg Shaka.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Shaka Hamdu Shaka,
akizungumza na wana CCM katika Shina Namba 6 Kijiji Cha Mnanje, katika
Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...