Na Mwandishi Wetu, Mtwara
KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka,
amekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika Wilaya za Masasi na
Newela mkoani Mtwara.
Mbali
na kutembelea miradi ya maendeleo, pia Shaka amepata nafasi ya kukutana
na wanachama wa CCM, pamoja na wanananchi kwenye vijiji mbalimbali
ndani ya Wilaya hizo ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea mikakati ya
Serikali katika kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo.
Shaka
ambaye yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi inayokwenda sambamba na
kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 pamoja na
kukagua Uhai wa Chama kuanzia ngazi ya mashina.
Akiwa
wilayani Masasi Shaka amekagua miradi ya maji katika eneo la Chidya
ambapo akiwa kwenye mradi huo amepata maelezo ya utekelezaji wa mradi
huo na kuelezwa utakamilika kwa wakati uliokusudiwa.
Baada
ya kutembelea mradi huo Shaka ametembelea Shule ya Sekondari Chidya
ambayo pia inawafunzi wenye mahitaji maalum na akiwa shuleni hapo
amepata nafasi ya kusikiliza kero za wanafunzi na kisha kuzitolea
maelekezo kwa Serikali ya Mkoa wa Mtwara.
Pia,
akiwa shuleni hapo Shaka amesikiliza kero zinazowakabili wanafunzi
wenye mahitaji maalum ikiwemo ya uhitaji wa baiskeli za watu wenye
ulemavu ili kuwasaidia kuwatoa sehemu moja hadi nyingine. Shaka ameahidi
kuwasaidia baiskeli hizo huku akiagiza kero nyingine zote kutafutiwa
ufumbuzi.
Katika
hatua nyingine Shaka ametembelea Shina la CCM lililopo kwenye Kijiji
cha Chiwata kilichopo ndani ya Wilaya ya Masasi na akiwa hapo Wananchi
waliopata nafasi ya kuzungumzia changamoto zinazowakabili wameomba
kutatuliwa changamoto ya maji, barabara na umeme.
Baada
ya kusikiliza changamoto hizo Shaka amewahakikishia Wananchi hao kuwa
Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itatafuta ufumbuzi wa
waharaka na tayari ametoa maelekezo kwa viongozi wa Mkoa wa Mtwara ili
wachukue hatua zinazostahili na Wananchi waondokane na kero hizo.
Shaka
katika ziara hiyo alitembelea soko la wafanyanyabiashara Masasi na
akiwa hapo amepata taarifa za uwepo wa tabaka katika kuwapanga
wafanyabiashara,hivyo ametoa maelekezo kwa viongozi wa halmashauri ya
Wilaya Masasi kuweka utaratibu mzuri utakaondoa malalamiko.
Wakati
huo huo Shaka amefanya ziara wilayani Newala kwa kukagua miradi ya
maendeleo na kuzungumza na wananchi pamoja na kusikiliza kero ambapo
baadhi ya kero alilazimika kuwasimamisha wakuu wa Idara kutoa ufafanuzi
na nyingine alimsimamisha Mkuu wa Mkoa.
Miongoni
mwa changamoto nyingi ambazo zimelalamikiwa na Wananchi ni miundombinu
mibovu ya barabara,kukosekana kwa maji na umeme kwa baadhi ya vijiji na
vitongoji na yote hayo Shaka amewaahidi kupatiwa ufumbuzi wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...