Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Makatibu Mahsusi wa Ofisi mbalimbali za Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) kwa ajili ya Makatibu hao nchini katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama, akimakabidhi cheti Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Martha Mashiku, kama ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kufadhili Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) kwa ajili ya Makatibu hao nchini katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma.
Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Martha Mashiku, akitoa mada kuhusu fursa zinazotokana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na kampuni ya uwekezaji ya UTT wakati wa Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), wakipata maelezo kuhusu fursa zinazotokana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na kampuni ya uwekezaji ya UTT.
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wafadhili wa Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...