Na Mwandishi wetu Loliondo.

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro leo  amefanya ziara katika eneo la Loliondo, Ngorongoro kwa ajili ya kujionea zoezi linaloendelea la uwekaji alama za mipaka, ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na kasi iliyopo.

IGP Sirro ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella, amewataka washiriki wa zoezi hilo kujituma ili kazi ya uwekaji alama za mipaka katika eneo hilo iishe kwa wakati.

Sirro amesisitiza wananchi kuwa watulivu na kushirikiana na serikali katika uamuzi huu wenye lengo la kuhifadhi eneo hilo kwa faida mtambuka za nchi.

'Msikubali kutumika kuchochea vurugu ambazo hazina manufaa kwa pande zote  na wala msikubali kutumika kwa niaba ya wale wote wasiotutakia mema kama taifa', alisema Sirro.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella alimhakikishia IGP Sirro kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imejipanga kuhakikisha kuwa zoezi linaendeshwa kwa hali ya utulivu kwa kuzingatia sheria za nchi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...