Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Wizara ya Maliasili na Utalii iko tayari kutoa ushirikiano kwa wadau wanaofanya jitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuandaa matamasha ya kutangaza utalii wa utamaduni na malikale.

Ameyasema hayo leo Juni 13, 2022 ofisini kwake jijini Dodoma alipokutana na waandaaji wa tamasha la Nandete Majimaji Festival litakalofanyika kuanzia tarehe 13 mwezi Agosti 2022 na kumalizika 15 mwezi Agosti 2022 katika Kata ya Kipatimo Kijiji cha Nandete Mkoani Kilwa.

Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya “ Majimaji Tujiandae Kuhesabiwa ”litahusisha mashindano ya mbio, mashindano ya mpira wa miguu na mashindano ya ngoma za asili ambapo washindi watapewa zawadi mbalimbali.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...