BALOZI
wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesema katika kuendeleza
mahusiano mazuri na Tanzania wataendelea kuongeza idadi ya wanafunzi wa
kitanzania watakakwenda kusoma masomo ya shahada za Awali, shahada za
Umahiri na Uzamivu nchini Ufaransa ili kitimiza azma ya kubadilishana
Teknolojia na ubunifu baina ya nchi hizo.
Ameeleza
hayo wakati hafla ya dhifa iliyowakutanisha wanafunzi waliowahi kusoma
nchini Ufaransa (Alumni,) pamoja na wanafunzi watatu waliopata ufadhili
wa masomo nchini Ufaransa kuanzia mwezi Septemba.
Balozi Nabil amesema wanafunzi watanzania watumie fursa hiyo ili kuleta tija kwa Taifa.
"Serikali
ya Tanzania imejikita katika uwekezaji na Rais Samia Suluhu Hassan na
Rais wa Ufaransa wamedhamiria hilo mara baada ya kukutana na wawekezaji
kutoka Ufaransa wameshaanza kuja Tanzania kupitia kampuni kubwa na za
kati ambazo zinahitaji wataalamu... wanafunzi wafuatilie fursa hizi za
masomo ambayo watayasoma kwa kiingereza na waweke nia katika hilo.
Balozi
Nabil amesema, wamekuwa wakitembelea vyuo mbalimbali nchini na kueleza
fursa mbalimbali za masomo na ujuzi wanazoweza kuzipata kupitia ubalozi
wa Ufaransa nchini.
Mmoja
ya wanufaika wa fursa ya masomo Mathew Choaji ambaye atakwenda kusomea
masuala ya dawa na Vifaa Tiba amesema, fursa hiyo italeta tija kwa jamii
hasa katika sekta ya afya.
Amesema,
kwa wakati huu ambao Serikali imejikita katika uwekezaji ikiwemo ujenzi
wa viwanda vya dawa italeta wataalamu wazawa katika kuviendesha kwa
faida ya watanzania.
Mtandao
wa Alumni wa Ufaransa una zaidi ya wahitimu wapatao 340,000 waliojisali
kote duniani huku Tanzania ikiwa na wanachama 400 waliosajiliwa kupitia
Tanzania Francealumni.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil
Hajlaoui akizungumza wakati wa hafla ya doing iliyowakutanisha wanafunzi
watanzania waliowahi kusoma nchini Ufaransa pamoja na wanafunzi watatu
waliopata ufadhili wa masomo nchini Ufaransa kuanzia mwezi Septemba
mwaka huu, Balozi ameeleza kuwa wataendelea kuongeza idadi ya watanzania
watakaokwenda kusoma nchini Ufaransa.
Balozi
wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui akizungumza wakati wa hafla
ya doing iliyowakutanisha wanafunzi watanzania waliowahi kusoma nchini
Ufaransa pamoja na wanafunzi watatu waliopata ufadhili wa masomo nchini
Ufaransa kuanzia mwezi Septemba mwaka huu, Balozi ameeleza kuwa
wataendelea kuongeza idadi ya watanzania watakaokwenda kusoma nchini
Ufaransa.
Mwanafunzi
aliyepata fursa ya masomo nchini Ufaransa Mathew Choaji akizungumza
wakati wa hafla hiyo na kuahidi kuitumia vyema fursa hiyo kwa manufaa ya
jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...