Picha kutoka jijini Los Angeles nchini Marekani wakati Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa alipo udhuria tamasha la utoaji tuzo za BET kwa mwaka 2022, lililofanyika usiku wa kuamkia June 27 katika ukumbi wa burudani (arena) wa Microsoft theater.
Katika
ziara hiyo Waziri Mchenegerwa ameambatana na Katibu Mkuu Dkt. Hassan
Abbasi pamoja na Mkurugenzi wa Sanaa dkt. Emmanuel Ishengoma katika
kutafuta ujuzi wa namna ya kuandaa tuzo kwa kiwango cha kimataifa, lengo
likiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuitangaza Tanzania wakati
ambapo Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa tuzo za MAMA – MTV African
Music Awards 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...