Na WMJJWM-Dodoma
Wadau wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kupitia mradi wa Mtoto Kwanza wamejipanga kujikita kutoa elimu ya Malezi kwa jamii ili isadie kuondokana na mmomonyoko wa maadili unaochangia kutokea kwa vitendo vya ukatili.
Hayo yamebainika jijini Dodoma wakati wa kikao kilicho wakutanisha wadau hao kwa lengo la kuwapitisha kwenye Mradi huo katika utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto.
Mkurugenzi wa Shirika la Bright Jamii Initiative Irene Fugara alisema Shirika lake limejikita kuhakikisha linatoa elimu ya Malezi kwa Mtoto ili kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya Watoto ili iweze kusaidia kuondoka na tatizo hilo.
"Lazima tuijengee jamii uwezo wa kuwa na uelewa kwenye masuala ya Malezi ili iwasaidie katika kuhakikisha watoto wanalelewa kwenye mazingira mazuri na yatakayowawezesha kuwa wazalendo, jasiri na wenye kujiamini " alisema Irene
Naye Meneja Programu kutoka Shirika la KIHUMBE Jeremia Henry amesema Shirika hilo linashirikiana na Serikali na wadau wa maendeleo hasa upande wa miradi ya watoto na vijana katika masuala ya Afya, Malezi, Makuzi, na pamoja na Lishe ndani ya jamii.
"Kupitia Programu hii Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto tumepata uelekeo utakaotusaidia kuona ni namna gani tutatoa elimu ya Malezi kwa jamii ili tuwe na jamii yenye watu wenye Malezi bira" alisema Jeremia
Akifungua kikao hicho Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku alisema Serikali imeweka jitihada mbalimbali ili kuhakikisha jamii inapata elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa kuzindua Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto inayolenga kusaidia kutoa elimu ya Malezi chanya ndani ya jamii.
Mkurugenzi huyo alisema pia uwepo wa Programu hiyo nchini utasaidia kujiamini kwa kujenga kizazi chenye kung'amua changamoto mbalimbali katika jamii na kuzifanya fursa za kimaendeleo katika jamii husika.
"Programu hii imeandaliwa na kuzinduliwa kwa lengo la kuziba mapengo yaliyopo kwa sasa, kwakua na mipango na Programu zingine za Malezi kwa Mtoto, hivyo itasaidia kutatua changamoto ziliziokuwepo miongoni mwa jamii hasa kwenye Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto " alisema Kitiku.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Mkurugenzi wa Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Mwajuma Rwebangira alisema lengo la kikao hicho ni kuwapitisha wadau wa Mradi wa Mtoto Kwanza katika Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ili waweze kutumia Programu hiyo katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto.
"Sisi wadau wa Mtoto Kwanza katika kutekeleza mradi huu tuhakikishe tunatumia Programu hii ili kuhakikisha tunajikita katika kutoa elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto katika sehemu tunazotoka" alisema Mwajuma
Mkurugenzi wa
Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku akizungumza na wadau wa
Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwenye Programu Jumuishi
ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto wakati wa kikao
kilichofanyika
jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...