MKUU
wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, amesema kwa hakika Serikali ya
awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,imeitendea haki Wakala
wa barabara za Vijijini na mjini (TARURA )kwa kutenga fedha za
utekelezaji wa miradi kiasi cha sh Bilioni 44.650.6 kwa mwaka wa fedha
2021/2022.
Kati ya fedha
hizo Bilioni 21 .111.6 Ni kwa ajili ya mradi wa barabara ya lami Visiga
-Zegereni na Bilioni 1.367.387.2 kwa Ajili ya miradi ya dharura Kibiti ,
Mkuranga,Kibaha na Bagamoyo.
Akikagua
miradi ya barabara Viuatilifu,TAMCO -MAPINGA ambayo ipo chini ya
TANROADS , barabara ya kuelekea hospital ya Lulanzi,Tanita kuelekea chuo
cha uongozi cha CCM na Visiga -Zegereni , Kunenge aliwataka wakandarasi
wazitendee haki fedha hizo nyingi zinazotolewa na Serikali kwa
kutekeleza miradi kwa wakati bila ubabaishaji .
"Fanyeni
kazi usiku na mchana, kama umepewa tenda ya kuwa mkandarasi manake
umeaminiwa, tekelezeni kazi kwa wakati na kama kuna vikwazo
mnijulishe,:Sitaki kusikia changamoto ya mvua kwani wakati unapewa tenda
hii hamkujua kama kuna mvua!?alihoji.. Kunenge
Mmeaminiwa onyesheni uwezo wenu.
Alieleza
,TARURA na TANROADS Wana mahusiano mazuri ya kiutendaji kazi wanafanya
kazi kubwa ,ambapo kwa TARURA imeshapelekewa asilimia 95 ya fedha zote.
Kunenge alifafanua,kwa TANROADS ilitengwa zaidi ya sh.bilioni 42 na Hadi Sasa wameshapelekewa asilimia 75 ya fedha hizo.
"Tunamshukuru
Rais wetu,mkoa kautendea haki ,Kwa upande wa barabara hii ya Visiga
-Zegereni Ni mradi unaokwenda Viwandani km 12.5 unatekelezwa na TARURA
,Sasa utaona mradi huu unagharimu Bilioni 21 Hadi kukamilika Ni Jambo la
faraja kwakuwa utasaidia wawekezaji kusafirisha malighafi na bidhaa zao
kwa urahisi"alisisitiza Kunenge.
Awali Meneja wa TARURA mkoa ,Leopold Runji alisema mradi wa Visiga- Zegereni umefikia asilimia 10 Hadi Sasa.
Alisema ,wametengewa Bilioni 44.6 na wameshapokea Bilioni 25.074.3 .
Runji
alitaja mafungu ya fedha walizopokea kimkoa Kuwa ni Pamoja na mfuko wa
barabara Bilioni 8.2 kwa Ajili ya matengenezo ya barabara ya kawaida
kilometa 873.98 , Mfuko wa Jimbo Bilioni 4.8 na Miradi ya fedha za tozo
Bilioni 28.236.6 .
Dereva
bodaboda Majid Muhammad alisema kwasasa wanapata changamoto kipindi cha
mvua hivyo wanashukuru Serikali kwa mipango ya kuboresha barabara Hali
itakayowawezesha kupita kwa urahisi .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...