Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Nachingwea
SITAMUANGUSHA Rais Samia! Ndivyo anavyoeleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kueleza kwamba atahakikisha anatumia akili zake, nguvu zake na maarifa yake yote kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kutumiza malengo yake katika kuwatumikia wananchi wote na kuwaletea maendeleo.
Akizungumza mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka pamoja na wanachama wa Chama hiko Mkoa wa Lindi, Waziri Mkuu amesema tangu Rais Samia amemtua kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hajawahi kuzungumza lakini leo ameona ni vema akasema kuhusu uteuzi wake baada ya kuaminiwa na Rais Samia.
"Naomba nitamke hili mbele ya wana Lindi wenzangu, tangu Rais Samia ameingia madarakani na kuridhia mimi kuendelea na nafasi hii sijawahi kutamka, nataka kumshukuru yeye kwa kutuamini wana Lindi. Nawashukuru wana Lindi kwa uvumilivu wenu maana kuna wakati huwa sipatikani, lakini naomba niwaahidi nitaendelea kufanya kazi kwa karibu na Rais Samia..
“Namuahidi Rais Samia nitamsaidia kwa nguvu zangu zote, uwezo wangu wote kuhakikisha tunafanikisha malengo yake, wana Lindi tuendelea kumuunga mkono Rais na kila anachofikiria basi tuwe wa kwanza kumsaidia," amesema.
Amesema wana Lindi wanayo kila sababu ya kuwa wa kwanza katika kuunga mkono maono ya Rais Samia katika kuwatumikia Watanzania kwani amewapa heshima kubwa wana Lindi kutokana na nafasi ambayo amepewa na Rais.
Waziri Mkuu amesema Mkoa wa Lindi sasa una mabadiliko kutokana na jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia serikali inayoongozwa na Rais Samia.
"Wana Lindi nataka kuwaambia fursa ambayo tumeipata wana lindi ya kuheshimiwa ya kupata mtumishi wa kumsaidia kazi mheshimwa Rais kutoka miongoni mwetu wana Lindi, na mimi namjua vizuri kwa umahiri wake, uwezo wake na hata anapotoa maelekezo mkoa wa Lindi nao umekuwa ukiguswa," amesema.
Amesema kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM inayosimamiwa na Rais Samia, sisi tuwe watu wa kwanza kutekeleza, "jukumu letu ni kumsemea, jukumu letu kumuunga mkono, wote ambao tuko hapa tufahamu Rais Samia ndio kiongozi wetu, tutaendelea kumuunga mkono kwa kila hatua."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...