Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

WANANCHI, Yanga SC wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC Premier League) baada ya kupata ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Coastal Union FC ya Tanga na kufikia alama 67 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote inayoshiriki Ligi hiyo ya Tanzania.

Yanga SC wamejihakikishia ubingwa mbele ya Coastal Union kwa mabao ya Mshambuliaji Fiston Mayale dakika ya 34 na 68, Chiko Ushindi dakika ya 52, kwenye mchezo huo.

Yanga SC wamecheza kipindi cha kwanza bila kupata bao, kipindi cha pili walibadilisha mchezo na kupata ushindi huo wa mabao 3-0 dhidi ya Wagosi wa Kaya.

Yanga SC wanaondoka na kitita cha Shilingi Milioni 600 jumla, ikiwa Shilingi Milioni 500 za Mdhamini wa Ligi hiyo Azam Media na Shilingi Milioni 100 kutoka kwa Mdhamini Benki ya Biashara (NBC Bank).


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...