Na Khadija Seif, Michuzi TV
MABONDIA wawili Seleman Kidunda na Erick Tshimanga Katompa wamepima uzito na kutarajiwa kupanda ulingoni kuwania ubingwa WBF katika pambano litakalopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji Songea Mkoani Ruvuma.
Mabondia hao wamepima uzito katika eneo stendi ya daladala ya Mfananyaki iliopo mjini Songea ambapo pambano hilo linasubiriwa kwa hamu sambamba na Karim Mandonga anayetarajia kupanda ulingoni dhidi ya Shabani Kaoneka ambao watacheza pambano la utangulizi.
Kidunda na Katompa watapanda ulingoni katika pambano hilo ambalo litapigwa kwa raundi kumi kwenye uzani wa Super middle.
Mabondia hao mara baada ya kupima uzito kila mmoja amemtambia mwenza akidai atahakikisha anaibuka na ushindi katika pambano.
Kidunda ameeleza kuwa ataleta ushindi nyumbani mashabiki waondoe hofu.
“Watanzania nipo vizuri na sina presha ninachotaka kuwaambia ni kwamba nitampiga kwa sababu hao Wakongo wamezoea kuongea halafu hayo mimi siyawezi, njooni kwa wingi Majimaji muone burudani,”.
Kwa upande wa Katompa amewashukuru wakazi wa mjini wa Songea kwa mapokezi ambayo ameyapokea huku akiahidi kuonyesha mchezo mzuri katika pambano hilo.
Wapinzani wawili kati ya Bondia wa Ngumi za kulipwa kati ya Selemani Kidunda na Erick Katompa kutoka Kongo wakitunishana misuli mara baada ya kupima uzito uliokamilika kilo 76 Kwa pande zote mbiliBondia wa Ngumi za kulipwa Karim Mandonga akipima uzito kuelekea pambano la payback dhidi ya mpinzani wake Shaban Kaoneka litakalopigwa uwanja wa Majimaji Songea Mkoani Ruvuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...