Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 29, 2022 wakati wa kutangaza kuanza kusughulikia kero na Malalamiko ya migogoro ya Ardhi 975 iliyopo nchini. Kulia ni kamishna msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam, Idris Kayera
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 29, 2022 wakati wa kutangaza kuanza kusughulikia kero na Malalamiko ya migogoro ya Ardhi 975 iliyopo nchini.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
LICHA Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupewa jukumu ya kusimamia Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayosimamia masuala ya ardhi nchini, sasa kukutana na wakazi wa jiji la Dar es Salaam ili kusikiliza malalamiko au kero za Migogoro ya ardhi iliyopo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 29, 2022, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi amesema watasikiliza wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa siku tano mfululizo kuanzia Agosti Mosi hadi Agosti 5.

Utaratibu huo unawahusu wale ambao wameshawasilisha kero zao kwa maandishi kwenye ofisi ya Mkoa, au Wizarani.

“Walalamikaji wote wanaombwa kuwasilisha kero zao wakiwa na vielelezo vyote vitakavyosaidia Kamati kutatua malalamiko au kero kwa haraka.” Amesema Dkt. Kijazi

Amesema Uongozi wa Wizara umeamua kuweka nguvu ya kipekee kwenye kutatua kero na Malalamiko ya migogoro ya ardhi kwa kuanzia na mikoa ambayo migogoro ni mingi.

Amesema kuwa Wizara hiyo imekuwa ikipokea malalamiko mengi ya migogoro ya ardhi, hasa inayohusu umiliki wa viwanja kwenye Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha na Mbeya. Pamoja na jitihada za kutatua migogoro hiyo kwenye ngazi ya Mikoa, Wizara imebaini kwamba bado malalamiko ya wananchi yamekuwa ni mengi na mengine ya muda mrefu nayana wakatisha tamaa walalamikaji.

Dkt. Kijazi amesema kuwa sekta ya ardhi imekuwa ikigubikwa na migogoro ya mara kwa mara ambayo inazorotesha maendeleo ya mtu mmoja mmoja, jamii na nchi kwa ujumla ambapo wasingependa liendelee kuwepo Kutokana na unyeti wa suala la ardhi.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam wataanza kusikiliza kero na Malalamiko ya migogoro ya Ardhi katika wilaya zote kwa awamu huku wakiwa na Utaratibu mahususi Kwa tarehe zote hizo Kamati itakuwa kwenye jengo la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi lililopo Kivukoni Dar es Salaam.

"Tarehe 01/08/2022- Kupokea malalamiko kutoka Manispaa ya Temeke

Tarehe 02/08/2022- Kupokea malalamiko kutoka Manispaa ya Kinondoni

Tarehe 03/08/2022- Kupokea malalamiko kutoka Manispaa ya Kigamboni

Tarehe 04/08/200 – Kupokea malalamiko kutoka Manispaa ya Ubungo

Tarehe 05/08/2022 – Kupokea malalamiko kutoka Jiji la Ilala." Ameeleza Dkt. Kijazi.

Ili kuhakikisha kwamba sekta ya ardhi inachangia kikamilifu kwenye maendeleo ya nchi yetu, Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kutatua migogoro hiyo.

Dkt. Kijazi amewaomba wananchi kufika katika Jengo la Wizara hiyo lililopo Kivugoni, Magogoni jijini Dar es Salaam, kupeleka malalamiko yao ili kuyapatia ufumbuzi wa kimaandishi na kama Mwananchi asiporidhika aende na maandishi hayo katika hatua inayofuata.

Awali Dkt. Kijazi Amesema kuwa Serikali iliweka nguvu kwenye kutafuta ufumbuzi wa changamoto za migogoro mikubwa na ili kufanikisha zoezi hilo Rais Samia aliunda Kikundikazi cha Mawaziri wa kisekta ili kutekeleza maamuzi ya Baraza ya Mawaziri kuhusu migogoro hiyo 975 mikubwa ambayo ilishafanyiwa kazi.

Wizara zinazohusika na utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kwa migogoro hiyo 975 ni Wizara ya Ardhi (Mwenyekiti), Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Ulinzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...