Na John Wallter-Babati
Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Daniel Sillo ameendelea na ziara yake katika kata na vijiji mbalimbali Jimboni humo kutoa mrejesho baada ya vikao vya Bunge na kusikiliza kero za wananchi.
Aidha Sillo ametumia ziara hiyo kuwahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23,2022.
Akizungumza na wakazi wa vijiji vya Maganjwa,Sabilo kata ya Dabil, Mbunge Sillo amesema serikali ya awamu ya sita itaendelea kuwahudumia wananchi Kama ilani ya chama Cha Mapinduzi inavyoeleza.
Aidha Sillo amesema kushirikiana na TANESCO wataendelea kufikisha huduma za umeme katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa huku Afisa uhusiano wa TANESCO Marcia Simfukwe akieleza watatembelea makazi ya watu na Taasisi za Serikali na nyumba za ibada kuunganisha huduma za umeme katika kata hiyo.
Kwa upande wa Barabara na maji Mbunge huyo amesema huduma hizo zitaendelea kutolewa na kwamba amepata mfadhili atakayechonga Barabara ya Kijiji Cha Maganjwa hadi Shule za Msingi Sekondari ya Maganjwa huku RUWASA wakieleza kuwa wanaendelea kusambaza huduma za maji maeneo yote ya vijijini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...