Raisa Said,Korogwe.


MBUNGE wa Korogwe Vijijini Mkoani Tanga, Timotheo Mzava ameiomba Serikali ijenge kituo maalumu cha askari wa wanyamapori ili iwe rahisi kupambana na tembo katika Wilaya hiyo.

Ombi hilo amelitoa juzi jioni mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja wakati wa ziara yake ya kuelezea ufumbuzi wa muda mfupi uliochukuliwa na Serikali wa kudhibiti tembo katika maeneo ya makazi na kwenye mashamba ya wananchi na wawekezaji.

Mzava alisema tembo wamekuwa ni changamoto kubwa katika kata 10 zilizopo Tarafa ya Mombo na kwamba wamesababisha uharibifu mkubwa wa mazao katika mashamba ya wakazi wa maeneo hayo.

"Tembo wamekuwa ni tatizo kubwa kwenye wilaya yetu, mazao yanaharibika. Katika kata za Mkomazi na Mkumbara hawakuishia kwenye mazao tu, bali tembo hao wamesababisha vifo vya watu," alisema Mnzava.Licha ya Mbunge huyo kuomba kituo hicho, pia ametoa maombi mengine matano kwa ajili ya kudhibiti tembo hao, ikiwa pamoja na kutolewa kwa mafunzo ya ulinzi, kwa vijana wanaotoka katika vijiji husika.

Pia aliomba Mamlaka ya Wanyamapori (Tawa), Tawiri na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) wafanye utafiti wa kuangalia uwezekano wa kuweka uzio wa kutenganisha hifadhi na makazi ya watu ili wanyama wasitoke, huku pia akiomba
kifuta machozi kisichelewe nq kiongezwe.

Ombi lingine ni Serikali kupitia wizara ya Maliasili kubadilisha kanuni ya kifuta machozi ya mwaka 2011 ili kiendane na wakati.

Akijibu hoja hizo, Naibu Waziri Masanja alisema kuwa Serikali imefanya tathimini ikapanga iwe na suluhisho la muda mfupi na mrefu wa kutatua changamoto ya tembo.

Alisema wameanza kuyaainisha makundi ya tembo yanayotoka hifadhini ambapo watatumia mitambo ya kufuatilia wanyama walioko hatarini kupotea na kwamba mtambo huo uko kwa ajili ya faru lakini utatumika na kwa tembo.

"Mtambo uko kama televisheni na itasaidia Askari kuangalia na kufuatilia makundi ya tembo yanapoelekea. Pia tutawafunga Tambo kisukuma mawimbi ili iwe rahisi kufuatiliwa," alisema.Alisema wataweka kituo cha askari ili iwe rahisibkiwadhibiti wanyama hao.

Kuhusu kifuta machozi, Waziri Masanja ameagiza mpaka kufikia Agosti mifumo itakapofunguliwa wahakikishe wanawalipa wananchi wote waliofanyiwa tathimini pamoja na kuhakikisha tembo anayejulikana kwa jina la Maurana anadhibitiwa.

Alisema tembo wanavizia kipindi cha mavuno hivyo kipindi hicho wahakikishe ulinzi usio wakawaida unakuwepo ili kupunguza kadhia ya tembo huku akisisitiza Kwa kuwataka wahifadhi wafatilie ni wapi wameziba njia yao (shoroba) na kama ipo basi waichalie ili wasiweze kufika Kwa wananchi.

Awali wananchi wa kata ya Mkumbara, Magamba Kwalukonge na Mkaramo walimueleza Naibu waziri huyo kuwaHapa panaitwa Migombani lakini saivi hata mgomba mmoja hakuna na hata utumwe na mganga wa kienyeji hupati, hapa palikuwa panaitwa Miembeni, lakini hata embe moja hakuna, mpunga umeharibiwa minazi umeharibiwa utadhani katapila imepita," alieleza Mzee Mangale.

Mohamedi Ramadhani Maarufu Matofali alisema tembo wamewatawala wanawakosesha amani na kwamba Sasa hivi wanamadeninmakubwa sababu walikopa kwaajili ya kulima lakini tembo wameharibu mazao yote .

 






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...