WAIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amesema kuwa changamoto za wanajeshi zinaendelea kufanyiwa kazi na Wizara kwa kushirikiana na Makao Makuu ya JeAshi.
Mheshimiwa Waziri ameyabainisha haya wakati akiongea na Maafisa na Askari, alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea vikosi kanda ya Pemba vilivyo chini ya Brigedi ya Nyuki.
Kabla ya kuongea na Mafisa na Askari, Mheshimiwa Waziri alitembelea hivyo ambapo aliweza kupatiwa taarifa mbalimbali za utendaji wa vikosi hivyo, kuhusu historia ya vikosi, hali ya kisiwa, muundo, utendaji kivita, mafunzo, utawala, changamoto, hatua za kukabiliana na changamoto, mahusiano na taasisi nyingine za kiraia pamoja na mapendekezo.
Kabla ya kuhitimisha Ziara yake kisiwani humo, Mheshimiwa Waziri aliongea na maafisa na Askari wa Kanda ya Pemba katika bwalo la Kikosi cha Kambi ya Ally Khamisi, aliwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri wanayoendelea kuifanya ya kulinda amani ya kisiwa cha Pemba na mipaka yake baharini, kwa kuwa kambi hizo nyeti na ni za kimkakati.
Kuhusu changamoto, Mheshimiwa Waziri amewatoa hofu kuwa changamoto zote zilizowasilishwa kwake ni za jumla maana zinafanana na mengine aliyotembelea zikiwemu uchakavu wa iundombinu ya majengo, upungufu wa ikama, magari ya utawala na nyingine nyingi zimeendelea kutatuliwa hatua kwa hatua. Akitolea mfano wa baadhi ya utatuzi wa changamoto hizo ni pamoja na kuongezeka kwa bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 katika Mafungu yote matatu yaani Fungu - 57, Fungu 38 - NGOME pamoja na Fungu - JKT ambayo itasaidia kutatua changamoto zilizopo.
Kuhusu chanagamoto ya uhaba wa sare kwa wanajeshi, Mheshimiwa Waziri amesema changamoto hiyo imefanyiwa kazi baada ya Serikali kutoa pesa za kununulia kitambaa cha sare, wanajeshi kupimwa na kushonewa sare ambazo tayari zimeanza kugawawiwa kwa baadhi ya Maafisa na Askari
Aidha, Mheshimiwa Waziri amebainisha kuwa Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, inatambua na kuthamini kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Jeshi letu. Hivyo basi, Mheshimiwa Rais amedhamiria kwa dhati kutatua changamoto zilizopo na kutoa kipaumbele kwa vyombo vya Ulinzi na usalama.
Vile vile, Mheshimiwa Tax alitoa wito kwa Maafisa na Askari hao, kuendelea kuzingatia viapo vyao vinavyohusu Utii, uhodari na uaminifu wakati Serikali inaendelea kutatua changamoto zao.
ziara hii ni mwendelezo wa Ziara zake anazozifanya za kutembelea Kamandi, Brigedi, vikosi na viteule kujionea utendaji kazi wa maeneo haya, changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuona namna ya kukabiliana nazo. Ziara ya kwanza visiwani humo aliifanya kwa kutembelea Makao Makuu ya Brigedi ya Nyuki, vikosi na viteule Kanda ya Unguja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...