Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC)Yesaya Mwakifulefule akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimishwa kwa mbio za Korosho Marathon zilizofanyika katika Kiwanja Cha Nagwanda Sijaona leo mkoani Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack akimkabidhi  kikombe cha Ushiriki wa Korosho Marathon  Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC ) Yesaya Mwakifulefule leo katika Kiwanja cha Nagwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dustan Kyobya akishiriki mbio za Km 5 za Korosho Marathon zilizofanyika kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.


Na Chalila Kibuda, Michuzi  TV  Mtwara

 MKURUGENZI wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Yesaya Mwakifulefule amesema kuwa Korosho Marathon ni aina yake kutokana kuwa wadau wengi kuliko marathon zilizopita.

Mwakifulefule amesema hayo mkoani  Mtwara wakati Korosho Marathon  iliyofanyika katika Viwanja vya Nagwanda Sijaona mkoani humo.

"NIC imekuwa sehemu ya wadhamini kutokana kutambua michezo na ndio wadau wa bima kwa kukata katila mahitaji yanayohusian a na Bima"

Amesema kuwa michezo ya mbio ina imarisha afya kwa wakimbiaji na kuwa na nguvu kazi ya taifa inahitaji wa watu wenye afya.

Mwakifulefule amesema kuwa  NiC inatambua umuhimu wa mbio ndio maana tumekuwa wadau katika kudhamini.

Aidha amesema NIC ni shirika kubwa limeendelea kutoa elimu ya bima na zao la korosho kwa wa sasa lina bima la unyaufu  ambapo imepunguza kilio cha wafanyabiashara wa korosho.

Mkurugenzi Masoko na Huduma na Huduma na huyo  ameeleza kuwa NIC iko katika soko la bima hivyo litaendelea kuwafikia wadau kwenye bima kwani mahitaji ni mengi.
Picha ya pamoja ya wadau wa Korosho Marathon wakiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja Yesaya Mwakifulefule kwenye korosho marathon zilizofanyika mkoani Mtwara.


Picha mbalimbali kwenye bango  Ukuta wa NIC kwenye Korosho Marathon
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...