Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Geita Gold FC rasmi imetangaza usajili wa Golikipa wa Kimataifa wa Burundi, Arakaza MacArthur kutoka Klabu ya Lusaka Dynamos FC, ambaye amewahi pia kucheza vilabu mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Geita Gold FC inayoshiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) msimu huu, imetangaza usajili huo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii, huku wakithibitisha kumpa mkataba wa mwaka mmoja Mlinda lango huyo wa Burundi.
Golikipa huyo aliyekuzwa kulinda lango na LLB Académic FC ya Burundi, amewahi pia kucheza Klabu za Sports Club Villa ya Uganda, FC Dikhil ya Djibouti, Vital'O FC na Flambeau de l’Est FC zote za nchini Burundi, Kakamega Homeboyz FC ya Kenya.
Golikipa MacArthur anaungana na Makipa wengine wazawa waliopo kwenye Kikosi cha Geita Gold FC ambao ni Khomeiny Aboubakar, Sebusebu Samson na Aron Kalambo endapo kama hawataondoka Kikosini hapo.
Hadi sasa, Geita Gold FC tayari wametangaza usajili wa Mlinzi wa pembeni George Amani Wawa kutoka Dodoma Jiji FC, Mlinzi wa kati, Hussein Bakari kutoka Polisi Tanzania FC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...