RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mariam Mwinyi wamejumuika na Viongozi mbalimbali katika hafla ya chakula cha jioni walichoandaliwa na mwenyeji wao Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye na Mkewe Angeline Ndayubaha Ndayishimiye, Ikulu Bujumbura.
Rais Dk. Mwinyi yupo nchini Burundi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi zitakazofanyika tarehe: 01 Julai, 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...