Na Mwandishi Wetu

Katika kuhakikisha Sera ya uhifadhi wa mazingira inatekelezwa kwa vitendo Shirika la Taifa la Madini(STAMICO) limeanza rasmi kupeleka bidhaa ya mkaa mbadala kwa wananchi kwa ajili ya matumizi ya majumbani.

Akizungumza katika Mahojiano na waandishi wa Habari yaliyofanyika leo Julai 1,2022 katika maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam Meneja wa Masoko na Uhusiano wa STAMICO Geofrey Meena amesema kuwa kwa sasa bidhaa hiyo imeeanza kuuzwa na kwamba mpaka sasa tayari wameshapokea maombi mbalimbali ya mawakala kwaajili ya kusambaza bidhaa hiyo nchi nzima.

"Tumekuja hapa Sabasaba na bjdhaa yetu ya mkaa mbadala pamoja na mambo mengine, lakini tunataka kuwaeleza wananchi kwamba sasa bidhaa hii inapatikana hapa kweye maonesho, uzalishaji unafanyika katika kiwanda chetu kilichopo TIRDO Msasani na tunaenda kuandaa utaratibu wa kuwapata mawakala watakaosambaza mkaa huu nchi nzima" amesema Meena.

Na kuongeza kuwa "Mkaa huu ni mkombozi kwa wananchi kwani unaweza kutumika kidogo kwa matumizi ya siku nzima na utasaidia sana kupunguza uhalibifu wa mazingira unaotokana na kukata misitu " ameongeza.

Aidha amesema kuwa katika maonesho ya mwaka huu STAMICO wamekuwa na banda lao wao wenyewe ikishirikiana na baadhi ya Taasisi kutoka Sekta Binafsi zinazojihusisha na uchimbaji wa Dhahabu pamoja na kiwanda cha kusafisha Dhahabu kiichopo Jijini Mwanza.

Amezitaja Taasisi zilizoshirikiana na na STAMICO katika maonesho hayo ni pamoja na Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya Buckreef Mining Company, Buhemba Gold Mining na Kiwanda cha Mwanza Precious Metals refinery Limited cha Jijini Mwanza.

Kwa upande wake Mhandisi Mtaalamu Uchenjuaji Madini kutoka STAMICO Happy Mbenyange anayesimamia bidhaa hiyo amesema kuwa uzalishaji wa Bidhaa hiyo unakwenda vizuri ambapo kwa sasa mtambo wao una uwezo wa kuzalisha tani mbili kwa saa na kwamba wanatarajia kupokea mitambo mingine kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Pia amesisitiza kuwa bidhaa hiyo ipo kwa wingi hivyo wananchi wanaweza kufika kwenye maonesho hayo ni kujipatia kwa bei nafuu.

"Mkaa upo wa kutosha na unapatikana hapa sabasaba wananchi wanaotembelea Maonesho haya wafike kwenye Banda letu la STAMICO kupata bidhaa hii kwa bei nafuu" amesema happy.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa STAMICO  Deusdedith Magala akiwa katika kikao na wadau mara baada ya kutembelea Banda la STAMICO Sabasaba.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu  wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) Deusdedith  Magala akizungumza na Mhandisi Pili Athumani katika banda hilo kwenye maonesho 46 ya Biashara Kimataifa Sabasaba
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) Deusdedith  Magala akizungumza na baadhi ya watu waliofika kwenye banda hilo katika maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Ijumaa 1,2022 wa pili kutoka kulia ni Mhandisi Mchenjuaji Madini  Happy Manyange na kushoto ni Mhandisi Pili Athumani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...