Mkuu wa Wilaya wa Wialaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akimkabidhi fedha kiasi cha shilingi Laki mbili na Elfu Hamsini, Mshindi wa awamu ya kwanza katika mchezo wa 'Dai risiti ya EFD upate Pesa' Katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta jijini Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tegeta jijini Dar Es Salaam leo Julai, 25, 2022.
Mkuu wa Wilaya wa Wialaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akimkabidhi Tisheti Mshindi wa awamu ya kwanza katika mchezo wa 'Dai risiti ya EFD upate Pesa' Katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta jijini Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tegeta jijini Dar Es Salaam leo Julai, 25, 2022.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Kikodi Tegeta, Husna Nyange akizungumza na mshindi wa leo Julai 25,2022 katika shindano la 'Dai risiti ya EFD upate Pesa' kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe na kulia ni Kaimu Meneja Mkoa wa Kikodi Tegeta, Mazula Mtwale.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 25, 2022 wakati wa kumtangaza Mshindi wa shindano la 'Dai risiti ya EFD upate Pesa'la Mkoa wa Kikodi wa Tegeta jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kikodi Kinondoni, Edmund Kawamala.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Kikodi Tegeta, Husna Nyangeakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 25, 2022 wakati wa kumtangaza Mshindi wa shindano la 'Dai risiti ya EFD upate Pesa'la Mkoa wa Kikodi wa Tegeta jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kikodi Kinondoni, Edmund Kawamala akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 25, 2022 wakati wa kumtangaza Mshindi wa shindano la 'Dai risiti ya EFD upate Pesa'la Mkoa wa Kikodi wa Tegeta jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe amesema kuwa malengo waliyojiwekea ya kukusanya Kodi kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2021/2022 wamefanikiwa kwa asilimia 100.3 katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta.

Ameyasema hayo leo Julai 25, 2022 katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzanai (TRA) Tegeta wakati wa kuwatangaza washindi wa awamu ya pili wa mchezo wa Kubahatisha wa 'Dai risiti ya EFD Ushinde Pesa' unaoendelea kuchezeshwa katika Mkoa wa Kikodi wa Tegeta jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa kuomba risiti sasa hivi ni fursa.

"Kampeni hii ina lengo la kuongeza Elimu, ushawishi na watu wajue wajibu wao wenyewe kudai risiti halali yenye kiwango kile ambacho kinalingana na huduma uliyoipata." Amesema Gondwe

Licha ya hayo Gondwe amewashukuru wafanyabiashara wa Mkoa wa Kikodi wa Tegeta kutoa risiti pale wanapouza bidhaa mbalimbali na kuwawezesha wanunuaji kuingia kwenye mchezo wa kubahatisha na kujishindia Pesa.

"Leo tumekuja kuwapongeza wafanyabiashara ili watoe risiti, pia nawaasa kampuni zote na wafanyabiashara ambao hawajajiandikisha TRA wajiandikishe ili utambulike na kupata makadilio ya kodi yaliyo sahihi." Amesema Gondwe

Amesema kuwa wananchi washirikiane katika kulipa kodi ili kutimiza matwakwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kulipa kodi kwa hiari.

Kwa Upande wake Mshindi wa Awamu ya kwanza, Durusila Ntungu amewahamasish wanchini kudai risiti halali pale wanaponunua bidhaa ili kuingia katika mchezo wa kuhabatisha unaochezeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kujipatia Pesa.

"Tuwe tunadai risiti kwa sababu tunasaidia ujenzi wa nchi yetu, tunaweza kusaidia kujenga madarasa pale wanaposoma watoto wetu, kujenga hospitali pia tunamsaidia Rais wetu, Mama Samia kujenga nchi yetu." Amesema Durusila

Maeneo ambayo mwananchi anatakiwa kununua bidhaa na kudai risiti halali ili uingie katika shindano hili ni Tegeta, Goba, Mbezi Beach, Bahari Beach, Ununio, Mabwepande, Boko, Madale, Wazo, Mbopo, Salasala, Kunduchi na Bunju.

Mchezo wa kubahatisha 'Dai risiti ya EFD Ushinde Pesa' ulizinduliwa Julai 18, 2022 katika eneo la  Mbuyuni Salasala Mkoa wa Kikodi Tegeta jijini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...