Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,alhaj Abubakari Kunenge, ameungana na viongozi mbalimbali wa Wilaya,mkoa na dini kuadhimisha Siku ya Kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kuulinda uhuru wa Tanzania, ambapo huadhimishwa ifikapo Julai 25 ya kila mwaka.
Siku hii ya kuwakumbuka mashujaa huambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala maalum ya kuwaombea mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea amani nchi kutoka kwa viongozi wa dini.
Wakizungumza katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa ,Viongozi wa dini mkoa,akiwemo Sheikh mkuu wa mkoa wa Pwani, Hamis Mtupa amehimiza uzalendo ,umoja,upendo na mshikamano nchini ili kuwaenzi mashujaa waliopigania uhuru wetu.
Alieleza , amani na uzalendo ndio tunu ya Taifa ambapo inastahili kulindwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Nae Askofu wa kanisa la Harvest Pentecoste Emmanuel Mhina alieleza ,suala la kupigania amani Ni la kujivunia nchini .
Walimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kudumisha uhuru na kuilinda amani na upendo nchini pamoja na kusimamia maendeleo na kuinua uchumi nchini bila kupoa.
Pia viongozi walipongezwa viongozi Mkoani humo,kwa umoja na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu ya kimaendeleo mkoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...