Naibu Waziri Mary Masanja (Mb) amesema kuwa Serikali itahakikisha inapata ufumbuzi wa changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu wanaovamia Makazi ya watu hususan tembo.

Ameyasema hayo leo katika ziara ya kikazi alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) mjini Morogoro.
Amesema kuwa Serikali haifurahishwi na matukio ya wananchi kuuawa na tembo au kuliwa mazao yao.

“Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan haifurahii matukio ya tembo kuuwa watu kwa sababu uhai wa mtu hauwezi kurudishwa” Mhe. Masanja amesisitiza

Amesema moja ya mikakati ya kutatua changamoto hiyo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mbinu za kukabiliana na tembo.

Ameongeza kuwa njia nyingine ya kutatua tatizo hilo ni kuwavisha tembo viongozi kola maalum ili kuwawezesha Askari Uhifadhi kujua mwelekeo wa kundi la tembo.

Pia, amesema Serikali inaendelea kutafuta mbinu za muda mrefu za kutatua changamoto hiyo.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za kusikiliza changamoto za Taasisi na kuangalia utekelezaji wa majukumu yake iili kutafuta ufumbuzi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...