KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amezuru  kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Omari Ali Juma Chake chake Pemba na kutaka aenziwe kwa mazuri aliyoyapigania.

Akizungumza akiwa kaburini hapo kabla ya kushiriki dua ya kumwombea marehemu Dk. Omari, Shaka alisema mwaka huu  Dk Omari ametimiza miaka 21 tangu kutokea kifo chake  Aprili mwaka 2001, huku nchi ikitimiza miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi.

"Hapa sio sehemu ya kutoa hotuba, ujumbe wangu ni kwamba mwaka huu tunatimiza miaka 21 tangu Dk. Omari alipotutoka. Alikuwa nguzo muhimu kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, wakati wote na kwa nafasi zote alizoaminiwa alitimiza majukumu yake kwa uzalendo mkubwa.

"Wakati tukimkumbuka Dk. Omari Ali Juma nchi yetu inatimiza miaka 30 tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, huwezi kuzungumzia mafanikio ya demokrasia bila kumkumbuka Dk. Omari kutokana na jitihada alizozichukua. Tuyaenzi yale aliyoyasimia kwa maendeleo ya taifa," amesema.

Aidha, amesema wakati Watanzania wakimwombea Dk. Omari pia wamwombee Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameendeleza ndoto na za viongozi waliotangulia akiwemo Dk. Omari.

Awali akizungumza kabla ya Dua hiyo, mwakilishi wa familia ya Dk. Omari,  Zubeir Ali Juma alishukuru na kukupongeza kwa uamuzi wa Shaka pamoja na viongozi mbalimbali kwa kuendelea kudhuru kaburi hilo mara kwa mara.

Viongozi mbalimbali walishiriki Dua hiyo ambapo kwa upande wa Ofisi ya Mufti iliwakilishwa na Mratibu wa ofisi hiyo Pemba Sheikh Said Ahmad Mohamed.

Kwa upande wa Madhehebu ya kikristo yaliwakilishwa na Mchungaji Benjamin Nderingo Kisanga wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Pemba.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...