TIMU ya Snipers Pool yenye Makazi yake Mwenge Mpakaji jijini Dar es Salaam imeibuka Bingwa katika mashindano ya Pool ya Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni na hivyo kufuzu kuiwakilisha Kinondoni kwaenye fainali za mashindano ya Pool ya Nane nane yajulikanayo kama Planet “88” Pool Competitions 2022.
Timu ya Snipers ilipata Ubingwa huo wa Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni kwa kuifunga timu ya Tiptop 13 – 10 na hivyo kufuzu kucheza fainali za Nane nane mwaka huu zinazotarajiwa kufanyika Agosti 19 - 21, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Timu ya Tiptop yenye makazi yake Manzese Tiptop pamoja na kufungwa na Snipers Pool Klabu nayo ilifanikiwa kuingia kwenye moja ya vilabu viwili vinavyotakiwa kuwakilisha Mkoa wa kimichezo kwenye fainali hizo.
Nafasi ya tatu ya mashindano hayo ilichukuliwa na timu ya Machuma chuma yenye makazi yake Ubungo Kibangu ambayo pamoja na ushindi huo haikufuzu kushiriki fainali za Nane nane.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Wanaume, Seif Hamadi kutoka timu ya Tiptop alitwaa ubingwa wa mashindano hayo kwa kumfunga Abdallah Hussein 9 – 6 na hivyo kufuzu kushiriki fainali za Nane nane 2022.
Washindi wengine wa upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles) waliofuzu kushiriki fainali za Nane nane 2022 ni wale wote walioingia hatua ya robo fainaliambao ni, Abdallah Hussein, Mussa Mkwega, Ambele Steven, Abeid Dau, Jackson Steven, Abdul Kiande na Amos Boniphace.
Upande wa Mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanawake, Grace Shindika alichukua Ubingwa huo kwa kumfunga Jackline Tido na hivyo kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za Nane nane 2022.
Jacline Tito kwa kuchukua nafasi ya pili lakini pia nae alifuzu kushiliki kucheza mashindano ya Nane nane 2022 kwani nafasi zilizokuwa zinahitajika kwa Wanawake ni Mbili tu.
Fainali za Mashindano ya Nane nane 2022 zitafanyika Agosti 19 – 21,2020 baada ya kukamilisha mzunguko wa Mashindano ya hatua ya Mikoa kwa Ilala, Temeke na Morogoro.
Mchezaji, Jackson Steven kutoka timu ya Snipers ya Mwenge Mpakani Kinondoni Jijini Dar es Salaam akicheza dhidi ya mpinzani wake Abdul Kiande wa timu ya Tiptop Manzese wakati wa Fainali za Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni za kufuzu kushiriki Mashindano ya Nane nane yajulikanayo kama Planet 88 Pool Competitions 2022 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.Jackson Steven wa timu ya Snipers alishinda mchezo huo.
Mchezaji, Baraka Jackson kutoka timu ya Tiptop ya Manzese Kinondoni Jijini Dar es Salaam akicheza dhidi ya mpinzani wake Mussa Mkwega wa timu Snipers ya Mwenge Mpakani wakati wa Fainali za Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni za kufuzu kushiriki Mashindano ya Nane nane yajulikanayo kama Planet 88 Pool Competitions 2022 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.Baraka Jackson wa timu ya Tiptop alishinda mchezo huo.
Mchezaji, Mussa Mkwegan kutoka timu ya Snipers ya Mwenge Mpakani Kinondoni Jijini Dar es Salaam akicheza dhidi ya mpinzani wake Baraka Jackson wa timu ya Tiptop Manzese wakati wa Fainali za Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni za kufuzu kushiriki Mashindano ya Nane nane yajulikanayo kama Planet 88 Pool Competitions 2022 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.Baraka Jackson wa timu ya Snipers alishinda mchezo huo.
Mchezaji, Abei Dau kutoka Klabu ya Tiptop ya Manzese Kinondoni Jijini Dar es Salaam akicheza dhidi ya mpinzani wake Abdallah Hussein wa Klabu Snipers ya Mwenge Mpakani wakati wa Fainali za Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni za kufuzu kushiriki Mashindano ya Nane nane yajulikanayo kama Planet 88 Pool Competitions 2022 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.Abeid Dau wa Klabu ya Tiptop alishinda mchezo huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...