JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MFUKO WA UTAMADUNI NA SANAA TANZANIA
Simu: 026-2322129
Nukushi: 026 -2322126
Tovuti: www.michezo.go.tz
Baruapepe: km@michezo.go.tz
Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma,
S. L. P 25,
40481 DODOMA
25 Julai, 2022
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Mwenyekiti wa Bodi ya MFUKO wa Utamaduni na Sanaa Tanzania anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi ya Mtendaji Mkuu wa MFUKO wa Utamaduni na Sanaa Tanzania.
1.0 MFUKO WA UTAMADUNI NA SANAA
Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ilihuisha MFUKO wa Utamaduni na Sanaa mwaka 2020 ili kutekeleza Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 inayoielekeza Serikali kuanzisha Mifuko kwa ajili ya kuimarisha Sekta za Utamaduni na Sanaa. Lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kuleta mageuzi ya kisekta kupitia Mikopo, Mafunzo na Ruzuku kwa wadau wa Sekta ya Utamaduni na Sanaa nchini. Kwa Mujibu wa Katiba ya MFUKO wa Utamaduni na Sanaa Ibara ya 7, MFUKO huu utasimamiwa na kuendeshwa na Bodi ya Wadhamini kwa kushirikiana na Mtendaji Mkuu na Sekretarieti.
1.1 MTENDAJI MKUU-NAFASI 1
1.2 MUHTASARI WA MAJUKUMU YA MTENDAJI MKUU
Mtendaji Mkuu atawajibika katika utekelezaji wa majukumu ya kila ya siku ya MFUKO na atakuwa Katibu wa vikao vya Bodi, na kwa ridhaa ya Bodi anaweza kukaimishawadhifa huu kwa mtu mwingine atakayeona anafaa.
1.3 MAJUKUMU YA KAZI
1. Atawajibika kwa Bodi kwa mujibu wa Katiba ya MFUKO;
2. Kutengeneza mpango mkakati na kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Mfuko ili kuleta mageuzi ya kisekta kutokana na shughuli za mfuko;
3. Kuandaa programu za mafunzo ambazo zitaleta mapinduzi katika sekta ya Utamaduni na Sanaa;
4. Kuwa Afisa Masuhuli wa Mfuko na msimamizi mkuu wa masuala ya utawala na rasilimali watu;
5. Kuhakikisha fedha zilizokopeshwa zinarejeshwa kulingana na makubaliano.
6. Kufanya tathmini ya ukopeshaji na urejeshaji unavyofanyika na jinsi ya kuboresha. Pamoja na kutathimini masuala hayo ya mikopo, Mtendaji mkuu atahakikisha ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa majukumu mengine ya mfuko;
7. Kudumisha uhusiano mzuri na wafadhili wa Mfuko kupitia utekelezajiwa vipengele vya makubaliano ndani ya mikataba.
8. Kuhakikisha majengo na vifaa vya ofisi vinatunzwa na kuwa katika hali nzuri;
9. Kuitisha vikao vya Bodi katika muda uliopangwa na Bodi, ataandaa na kutunza kumbukumbu za vikao. Mtendaji Mkuu atafuatilia na kusimamia utekelezaji wa maazimio ya vikao na kutoa taarifa;
10. Kuhakikisha udhibiti mzuri wa fedha na mifumo ya uhasibu na kuwajibika na matumizi yote ya Mfuko; na
11. Kutekeleza Majukumu mengine kama ambavyo ataelekezwa na Bodi.
1.4 SIFA NA VIGEZO VYA MWOMBAJI
Uraia: Awe Mtanzania
Mwenendo: Awe na akili timamu na mwenye ari ya kutaka kuleta mageuzi katika sekta za Utamaduni na Sanaa kupitia Mfuko huu.
Elimu: Shahada ya uzamili/umahiri katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utamaduni, Sanaa, Masoko, Uchumi, Utawala, Uhasibu, Fedha, Sheria au Usimamizi wa Biashara (Business Administration)/ Biashara (Commerce) iliyojiimarisha katika Uhasibu au Fedha au Masoko au sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Taasisi inayotambulika.
Uzoefu kazini: Uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitano (5), kati ya miaka hiyo, mitatu (3) lazima iwe katika nafasi ya uongozi.
SIFA NYINGINE: - Awe na uelewa na uzoefu juu ya masuala ya biashara ya ukopeshaji, miradi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi;
- Awe muadilifu;
- Awe na stadi nzuri za mawasiliano na uongozi wa ushirikishaji;
- Awe na uelewa wa Sheria zinazohusu masuala ya Fedha na Utoaji Mikopo nchini;
- Awe na uwezo wa kuchambua masuala mbalimbali ya kifedha;
- Uzoefu katika usimamizi na uendeshaji wa Mifuko itakuwa ni sifa ya ziada.
1.5 AINA YA MKATABA: Mkataba wa miaka mitatu (3).
1.6 MSHAHARA: Kulingana na viwango na miongozo ya Serikali kuu.
1.7 ENEO LA KAZI: Dar es Salaam
1.8 MUHIMU KUZINGATIA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa wale tu walioko tayari kwenye utumishi wa umma;
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria;
iii. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika;
- Shahada, Stashahada, Astashahada, Cheti.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI.
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards).
v. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hatimatokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA;
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE);
vii. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria;
viii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 5 Agosti, 2022.
Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Aidha, maombi yote yatumwe katika baruapepe hii: mfuko.utamaduni@michezo.go.tz; au Ofizi za Mfuko zilizopo Uwanja wa Benjamin William Mkapa, Jijini Dar es Salaam.
Limetolewa na;
MWENYEKITI WA BODI
MFUKO WA UTAMADUNI NA SANAA TANZANIA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...