Na Pamela Mollel,Arusha

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyekiti na mwenyeji wa mkutano wa 3 wa dharura wa Baraza la mawaziri wa nchi zinazozalisha almasi Afrika unaotarajiwa kufanyika mkoani Arusha

Haya yameelezwa na waziri wa madini mh Dotto Biteko wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Arusha

Mkutano huo unaotarajiwa kuanza hapo kesho julai 29 mwaka huu katika katika kituo Cha mikutano Cha kimataifa Cha Arusha ambapo lengo la mkutano huo ni kuidhinisha nyaraka muhimu za marekebisho ambazo ni katiba ,kanuni na miongozo ya umoja huo pamoja na kuteua viongozi wa 3 sekretarieti ambao ni katibu mtendaji na manaibu wake wawili

Mh Biteko amesema katika kipindi hiki ambacho Tanzania ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo umekuwa ni heshima kubwa kwa Tanzania kuwajibika kwaajili ya maendeleo ya nchi wanachama hususani katika usimamizi wa madini ya almasi

Ameongeza kuwa katika uongozi wa Tanzania kuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wameweza kujifunza zaidi kuhusu usimamizi wa sekta ya madini hususani katika madini ya Almasi kwa nchi wanachama na wasio wanachama walipata nafasi ya kujifunza nchini Tanzania kuhusu namna walivyofanikiwa kuendleza wachimbaji wadogo wakimwemo waadini ya Almasi na madini ya dhahabu na namna serikali ilivyoweza kusimamia mnyororo mzima wa shughuli za madini

Pia Baraza la mawaziri wa nchi zinazozalisha almasi Afrika ( Afrikan diamond producers assosiation - ADPA) inajumuisha nchi 18 ambapo 12 ni wanachama na 6 ni waangalizi huku wanachama ni nchi zinazozalisha almasi ambazo zimefuata Sheria za ADPA za Sasa huku Tanzania Ikiwa ni miongoni mwao

Sambamba na hayo ameendlea kuwasisitiza Wadau wa sekta ya madini wakiwemo wanazofanya shughuli za uchimbaji wa madini ya Almasi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika agust 23 mwaka huu .

Waziri wa madini Dotto Biteko akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...