Na Karama Kenyunko Michuzi TV 
MHASIBU wa zamani Wizara ya Mambo ya Ndani Christina Kaale, amehukumiwa  kulipa faini ya sh. Milioni nane ama kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani  baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka manne yaliyokuwa yakiwakabili likiwemo la ubadhirifu wa sh milioni 15.2.

Hukumu hiyo imesomwa leo Julai 28, 2022  katika, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Ramadhani Rugemalila wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.

Pamoja na adhabu hiyo, mahakama pia imemtaka Christina kuilipa Wizara hiyo, kiasi hicho cha Sh. Milioni 15.2   anazodaiwa kufanya ubadhirifu pindi atakapomaliza adhabu ya take. 

Katika hatua nyingine, mahakama hiyo imemuachia huru aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo Edwin Makene baada ya upande wa mashtaka kushindwa  kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Rugemalira amesema mahakama imepitia ushahidi wa pande zote mbili na kuona kwamba, upande wa mashitaka umeweza kuthibitisha mashitaka dhidi ya Christina.

Katika kesi hiyo washtakiwa walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri pamoja na ubadhirifu wa fedha.

Amesema hakuna ubishi kwamba, fedha hizo zililipwa kwa mshtakiwa wa kwanza na ndiye aliyestahili kufanya marejesho ya jinsi zilivyotumika.

Hakimu ameongeza kuwa , kwa mujubu wa ushahidi wa mshtakiwa huyo, aliieleza fedha hizo baada ya kupewa, alimkabidhi mhasibu mkuu na ndiye baadaye alimpa nyaraka za kujaza marejesho ya matumizi ingawa hazikutumika kwa matumizi yaliyokusudiwa.

Kabla ya kupewa adhabu hiyo, Hakimu wa serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupàmbana na Rushwa (TAKUKURU), Nickson Shayo, pamoja na mambo mengine, aliiomba mahakama imuamuru mahitakiwa huyo alipe fedha ambazo zimefanyiwa ubadhirifu.

Katika kesi hiyo upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi saba amoja na vielelezo mbalimbali huku washitakiwa wakijitetea wenyewe.

Washitakiwa hao wanadaiwa Juni 19 mwaka 2015 katika Wizara hiyo, Ilala ,jijini Dar es Salaam, kwa kutumia risiti zilizokuwa na maelezo ya udanganyifu walijipatia sh milioni 4.4 kwa madai kwamba zilitumika kwa ajili ya chakula na viburudisho katika sherehe ya kuwaaga wafanyakazi wastaafu wa wizara hiyo.

Ikadaiwa katika tarehe hizo, wizarani hapo,washtakiwa hao kwa nia ya kudanyanya walitumia risiti zilizokuwa na maelezo ya uongo na kujipatia sh milioni 2 kwa madai kuwa zilitumika kwa ajili ya kulipia ukumbi na viti katika sherehe ya kuwaaga wafanyakazi wastaafu wa wizara hiyo wakati wakijua si kweli.

Pia washitakiwa hao kwa ubadhilifu walijipatia sh milioni 15 kwa ajili ya matumizi yao binafsi ,zilizofika kwao kulingana na nafasi zao za utumishi wa umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...