Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA,) katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Nape amepongeza utendaji kazi wa Mamlaka hiyo na kuitaka kutoka na azimio la kujenga ofisi rasmi
katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba ili kuongeza kasi zaidi ya
kuwahuduma wananchi pamoja na kukutana na wadau wa sekta hiyo.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari Nape Nnauye (Kulia,) akizungumza na viongozi wa TCRA mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka hiyo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari Nape Nnauye amepongeza utendaji kazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA,) na kuitaka kutoka na azimio la kujenga ofisi rasmi
katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba ili kuongeza kasi zaidi ya
kuwahuduma wananchi pamoja na kukutana na wadau wa sekta hiyo.
Nape
ameyasema hayo leo mara baada ya kutembelea banda la TCRA katika
maonesho 46 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea
jijini Dar es Salaam na kueleza kwa mahitaji ya watu kutoka TCRA ni
makubwa na tayari ameongea na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo
Biashara nchini (TANTRADE,) Bi. Latifa Khamis juu ya Mamlaka hiyo
kujenga ofisi katika viwanja hivyo ili kupunguza gharama sambamba na
kuwa ofisi maalumu itakayowakutanisha na wa wadau wengi zaidi na
kuwahudumia.
''Ninafurahi
kuona TCRA ikikutana na wadau mbalimbali kutoka katika magazeti na
redio na kuwahudumia pia wananchi wanafika hapa na kupata elimu
kuhusiana na majukumu ya TCRA, kupitia maonesho haya ni vyema mkatoka na
azimio la kujenga ofisi katika viwanja hivi vya maonesho...umuhimu wa
TCRA ni mkubwa sana hasa katika mawasiliano ambayo yanamgusa kila
mtanzania, kukiwa na ofisi hapa italeta nguvu zaidi katika kuwahudumia
wananchi na kupunguza gharama za eneo hili ambalo TCRA inakutana na
wadau wake na kutoa elimu kila mwaka.'' Amesema.
Waziri
Nape amesema TCRA wamekuwa wakifuata kanuni na taratibu na kuzisimamia
vyema katika kutoa huduma na kuwataka kuendelea na kasi hiyo kwa
kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma ya mawasiliano katika maeneo
yote nchini.
Pia
amesema kuwa katika maonesho hayo yanayokwenda na kauli mbiu ya
'Tanzania ni Sehemu Sahihi kwa Biashara na Uwekezaji' ni fursa kwa
waandishi wa habari kutangaza mambo makubwa yanayofanywa na Serikali ya
awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuvutia
kampuni za uwekezaji na wafanyabiashara kwa manufaa ya taifa pamoja na
kutumia fursa ya kampuni za nje zilizoshiriki maonesho hayo kwa
kuzitangaza ili kuvuta wawekezaji wengi zaidi.
Matukio mbalimbali wakati Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye alipotembelea banda na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA,) katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...