Ikiwa zimesalia siku chache kuelekea siku ya mbio za Kimataifa za CRDB Bank Marathon, uongozi wa klabu ya Yanga wakiongozwa na Mfadhili na Mdhamini Mkuu, Ghalib Salim
Mohamed (GSM) na Rais wa Yanga, Hersi Said waliunga mkono kwa vitendo kwa kufanya mazoezi ya pamoja katika Amsha Amsha
ya kuelekea Agosti 14. Walianza kwa matembezi ya kutoka Makao Makuu ya Benki ya CRDB hadi viwanja vya The Green Oysterbay.
Hapo awali pia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, AbdulMajid Nsekela akiambatana na
Wakurugenzi Watendaji washirika wa CRDB Bank Marathon kufanya matembezi ya kujiweka sawa kulekea siku ya kilele ya mbio hizo, ambapo pia waliweza kusimika bendera ya CRDB Bank Marathon katika viwanja hivyo ambavyo mbio hizo zitaanza na kuishia.














Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...