Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewataka Wanachama wa Chama hicho kutambua kuwa mzizi na msingi wa maendeleo kwenye maeneo mbalimbali unaanzia kwenye Mashina ya Chama hicho kwa kuwashirikisha Mabolozi wake kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yameelezwa Agosti 3,2022 na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Daniel Chongolo wakati wa ziara yake mjini Moshi katika tawi la Msasani, Shina namba 2 kwenye Kata ya Kaloleni.
Chongolo ameeleza umuhimu wa Ulinzi na Usalama kwenye maeneo ya Mashina kwa kuwashirikisha Mabalozi ambao ni Viongozi wa maeneo hayo, “Mashina ya Chama ni muhimu, hata kuongea mambo ya Ulinzi na Usalama kwenye maeneo yetu”.
“Hata kwenye miradi ya maendeleo kuna umuhimu wa kuwaalika Mabalozi wa Mashina kushiriki kwenye miradi hiyo, Sisi tunataka miradi iibuliwe kwenye ngazi ya chini, na ngazi ya msingi ni kwenye Mashina ili wao (Mabalozi) wapeleke kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa”, amesema Chongolo.
Chongolo ametoa mwito kuhakikisha Viongozi wote kutengeneza miradi ambayo inaendana na Wananchi sanjari na kupeleka fedha kwenye maeneo husika kutatua changamoto mbalimbali kwenye maeneo hayo.
“Mfano, inapelekwa Shilingi Bilioni moja kwenye Halmashauri husika yenye Madiwani 30, alafu ile Bilioni moja inaenda kugawanywa kwa Madiwani wote 30 ili kila mtu apate kiwango chake, sasa kuna eneo linapaswa kupata Shilingi Milioni 20 lakini anapelekewa Shilingi Milioni 90 kwa sababu fedha ilitakiwa kugawanywa sawa”,
“Kuna sehemu inapelekwa Shilingi Milioni 200 lakini inaenda Shilingi Milioni 90, kwa masuala kama hayo Serikali ipo makini katika udhibiti wa fedha na upotevu wa fedha zake za miradi mbalimbali, ndio maana tumeunda Vyombo mbalimbali kusimamia upotevu huo usiokuwa na tija”, ameeleza Chongolo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akifurahia jambo kutoka kwa Mwenyekiti Bi. Fatma Mgonja wa Shina namba 2, tawi la Msasani kata ya Kaloleni, Wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...