Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV-Bumbuli
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo ametoa maelekezo ya
kutaka Kiwanda cha Chai Mponde kuanza kufanya kazi ifikapo Septemba
mwaka huu ili wakulima wa Chai waanze kunufaika na uwepo wa kiwanda
hicho ambacho kimesubiriwa kwa muda mrefu.
Akizungumza leo mbele
ya wananchi, Katibu Mkuu wa CCM Chongolo amesema ameaambiwa kiwanda hiko
kila siku kiko kwenye majaribio tu na hakifunguliwi, hivyo umefika
wakati kuhakikisha kiwanda hicho kinafunguliwa na kuanza kufanya kazi.
“Nilikuja
kwa mara ya kwanza mwaka 2013 nikiwa msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana,mimi ndio niliandika taarifa kwenda kwa Rais Jakaya
Kikwete kuelezea umuhimu wa kiwanda hicho wakati huo. Haiwezekani sasa
zaidi ya nane tunahadithia kiwanda kuzinduliwa.
“Hili jambo
haliwezekani na halikubaliki , nimemsikiza Mkuu wa Mkoa, napongeza
msimamo wake wa kufunguliwa hiki kiwanda , msimamo wake naunga mkono na
nitamlinda kuhakikisha huo msimamo unatekelezwa , nimeambiwa wahusika
wanasema majaribio rasmi yataanza mwezi wa tisa na ufunguzi uwe mwezi wa
12.
“Hivi jamani si kuna watu wamekopa mbolea, si kuna watu
wameanza kukatakata chai na baada ya mwezi mmoja itaanza kuchumwa, sasa
watapeleka wapi?Kiwanda kifunguliwe mwezi wa tisa na kianze kupokea chai
na kuchakata , mwezi wa 12 iwe kuzinduliwa rasmi na wakati huo
tunakunywa chai.Hayo ndio mambo tunayoyataka”amesema Chongolo.
Ameongeza
hawawezi kuwa wanakwenda mbele wanarudi nyuma, hawawezi kuwa wanapiga
maki taimu kwenye mambo ya msingi ya wananchi , Rais amewaamini na kila
mmoja kwa nafasi yake atomize wajibu wake.
“Mimi nitakuwa wa
mwisho kuacha mzembe akitukwamisha kwenye mambo , tutamshauri mwenye
mamlaka ya kuchukua hatua ili tuachane naye tusonge mbele, wako
watanzania wengi wa kumsaidia Rais kwenda mbele kwa kasi na wale
wataoatukwamisha wala haitakuwa gharama kuwashusha,”amesema Chongolo.
Katika
hatua nyingine, Chongolo amesema kwenye elimu bado kuna changamoto ya
mtoto wa kike kwenda shule ni shida , hawapeleki mabinti
shule.“Changamoto ya madarasa imekwisha wanaotakiwa kwenda shule wote
wanakwenda lakini kuna mabinti hawajakwenda shule , takwimu zipo.
“Ndugu
zangu mtu yoyote anayemzuia mtoto kwenda shule awe wa kike na wa kiume
akimzuia anafanya kosa kisheria, mtoto wa kike ana haki ya kwenda shule
na kwenye huu mkoa wa Tanga imedhihirika watoto wa kike wakienda shule
wanakuwa watu bora kweli kweli , si mmeona wengi , msifanye makosa ya
kuwakosesha fursa hiyo.
“Waacheni wapate fursa ya elimu, siku
hizi hata wanaume wote wanataka wanawake wasomi ili wasaidiane kwenye
maisha, sasa msipomsomesha mnataka auolewe akiachika abakie na mateso
kwasababu atakuwa hana pakwenda,tunataka mabinti waende huko lakini
wakiwa msada kwa familia zao,”amesema Chongolo.
Wakati huo huo
Chongolo amewaaambia wananchi hao kuwa CCM imepewa dhamana ya kuongoza
nchi mwaka 2020 kwa fursa nyingine na awamu nyingine na dhamana hiyo ni
ya miaka mitano mpaka 2025, kwenye kuongoza nchi ukipewa dhamana hakuna
kubagua wananchi, wananchi wote ni lazima uwatumike sawasawa, uwatendee
haki , uhangaike na changamoto zao sababu dhamana uliyopewa ni ya wote
na sio watu wachache
“Ndio maana mimi na wenzangu tumekuja huku
kuonana na wananchi kuwasilikiliza kuwatembelea, na kuangalia njia
sahihi ya kutatua changamoto kwa haraka. Ndugu wananchi tuliahidi mambo
mengi kwenye Ilani ya mwaka 2020 , tuliahidi kwenye maji,kwenye umeme
tunaona nguzo zimepanda hadi huu.
“Umeme sio anasa ni huduma ,
tumeahidi kwenye barabara na barabara ya kwanza ni ya Soni mpaka Bumbuli
kilometa 22 lakini haitakiwi kuchukuliwa ya Bumbuli mpaka Soni pekee
inatakiwa iende Bumbuli ishuke Korogwe. Hiyo ndio barabara itakuwa
imekamilika, niwahakikishie barabara hii itajengwa.” Muonekano wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli likiwa katika hatua za mwisho kukamili
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo ya
mchoro wa jengo la Halmashauri ya Bumbuli kutoka kwa Msanifu wa Majengo
Yassin Mringo.Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akionesha Jambo
Kwenye mchoro wa jengo la halmashauri ya Bumbuli wakati wa ziara yake
katika Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga ikiwa ni muendelezo wa ziara zake
za kukagua Uhai wa Chama na kukagua, kusimamia na kuhimiza utekelezaji
wa wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025 .
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na
wanachama na wakazi wa shina namba 3 tawi la Ubiri, Lushoto mkoani
Tanga.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wanachama
na wakazi wa shina namba 3 tawi la Ubiri, Lushoto mkoani Tanga ikiwa
sehemu ya ziara yake ya kukagua uhai wa Chama na Kuhimiza utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...