Raisa Said,Bumbuli.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Kalisi Lazaro ametangaza kiama kwa wachimba
dhahabu na wenye mashamba ambao wamewapa wachimba dhahabu maeneo
katika jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto.
Lazaro ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa
ziara ya Mbunge wa Viti Maalum, Husna Sekiboko, amepiga marufuku watu
wenye mashamba katika eneo la Vuga kutoa mashamba kwa wachimba dhahabu
ambao wanachafua vyanzo vya maji na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo
hilo.
Mkuu huyo wa Wilaya pia amepiga marufuku serikali za vijiji katika eneo hilo kuacha mara moja kupokea suhuru kutoka kwa wachimba madini akisema kuwa fedha hizo ni haramu zinatokana na shughuii ambayo inachafua vyanzo vya maji na kutokana na kemikali ziatotumika kusafishia madini hayo kutiririshwa katika vyanzo na kuweka afya za wananchi hatarini.
Alisema kupokea fedha hizo kwa kisingizio cha watu hao kusaidia miradi
ya maendeleo ktika sehemu hizo si cha kweli kwa sababu fedha hizo
hazionekani.
“Tusidanganywe na kadarasa kamoja. Serikali ya Mama Samia haishindwi
kutujengeneza madarasa. alisema.
Alisema kuwa wazee wa zamani walijua maeneo hayo yana dhahabu lakini
waliacha kuchimba na kutunza vyanzo hivyo kwa sababu wanajua umuhimu
wa maji kuwa hayana mbadala. “Dhahabu inaweza kuchimbwa katika maeneo
mengine ambayo hayana vyanzo,” alisema.
Lazaro alisema kuwa aliwahi kupiga marufuku uchimbaji huo katika
maeneo ya Mponde, Funta na Vuga lakini amepata habari kuwa wamerejea
katika eneo la maeneo hayo.
Mkuu huyo aliwaagiza watendaji wa vijiji kuwakamata watu hao
wanaochimba dhahabu mara moja. “Nilikwisha zungumza nao hawa
(watendaji). Sasa mimi sitaleta polisi kwa sababu kazi hiyo mnaiweza .
Ninyi mnawaona kila siku wanapokwenda mkiwa ofisini mwenu. Wakamateni.
Na wale wenye mashamba waliowapa maeneo wachimba dhahabu nikikuta
shimo tu nitawakamata,” alionya Mkuu huyo wa Wilaya.
Akizungumza katika mkutano huo, Bi Sekiboko alieleza kusikitishwa na
kukerwa na hali hiyo ya uchafuzi wa maji kutokana na uchimbaji wa
dhahabu unaofanywa na watu wachache.
Alisema kuwa kuna hatari watu kupata kansa kutokana na kemikali
zinazotumika kusafishia dhahabu kutiririka katika vyanzo vya maji.
“Takwimu zinaonyesha kuwa tatizo la kansa katika eneo la Ziwa Victoria
bi kubwa kutokana na kemikali za kusafishia dhahabu kutiririka na
kuingia katika vyanzo ambavyo vinatiririsha maji kwenye Ziwa
Victoria,” alisema.
Alisema kuwa wakazi wa maeneo hayo wanawez kufanya shughuli nyingine
za kilimo na kupata kipato kikubwa lakini wakati huo huo kuhifadhi
vyanzo vya maji.
Naye Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), wilaya ya Lushoto,
Erwin Sezinga alisema maji yanayotumiwa na binadamu kutoka vyanzo
hivyo hayafai kwa matumizi ya binadamu.
“Waziri wa Maji alitoa fedha kwa ajili ya Mradi wa Maji lakini nimekaa
na maji hayo kwa wiki mbili na hayakubadilika. Ni dhahiri hayafai kwa
matumizi ya binadamu,” aiisema.
Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji Kishewa, Saumu Shengovi alisema kuwa
wametoa amri kwa watu ambao wana mashimo katika mashamba yao
kuyafukia.
Naye mkazi mmoja wa eneo hilo alisema kuwa watendaji wa vijiji ni
waoga na wanafiki kwa sababu wanaoshiriki katika biashara hiyo baadhi
yao ni viongozi . “Mtu wa kwanza kuuza madini ni mwenyekiti wa Chama
hivyo walikuwa hawawezi kumkabili bosi wao,” alisema.
Alieleza kuridhishwa kwake na hatu ambao Mkuu wa Wilaya anazichukua
kuokoa maisha ya wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Kalisti Lazaro
Mbunge wa Viti Maalum Mkao wa Tanga Husna Sekiboko




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...