Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KANISA Halisi la Mungu Baba lililoko Tegeta eneo la Namanga jijini Dar es Salaam Agosti 28,2022 kuanzia saa moja asubuhi limeandaa sherehe ya kumletea Matunda Chanzo Halisi ya Shamba lake ambapo waumini wa kanisa hilo pamoja na waalikwa 1000 wanatarajiwa kuhudhuria na kushiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari Kiongozi wa Kanisa hilo Baba Halisi amesema watu wote wanakaribishwa bila kusita na kwamba hawaendi kwenye sherehe hiyo kwasababu ya kumshukuru mtu bali wanakwenda kumshukuru aliyewaumba .
Amesema kuna mambo mazuri na makubwa yametokea katika Taifa letu ila hatumjashukuru aliyetufanyia hayo, Kitabu kinasema katika Kumbukumbu 28:47-48 " Kwa kuwa hukumtumikia Bwana,Mungu wako,kwa furaha na moyo wa kushukuru,kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote;
"(48) kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta Bwana juu yako, kwa njaa na Kwa kiu na Kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote ,naye atakuvika kongwa la chumba shingoni mwako,hata atakapokwisha kukuangamiza .Kwa ufupi ni kwamba ukitendewa mengi bila kushukuru Muumba wa kila kitu anaruhusu kongwa la chuma shingoni mwako,"amesema Baba Halisi.
Amefafanua nchi yetu imepona kwenye janga la Kimbunga Job,imepona milipuko ya magonjwa kama vile Corona ,njaa ,mgao wa umeme, ukame ,jangwa,maandamano ya vurugu mtaani, valcano na mengine mengi na Taifa limebakia kuwa salama .
"Kwa haya machache na mengine mengi ni vema wote bila kujali kusanyiko la dini au dhehebu lako, tuje kumshukuru aliyetuponya kwa mujibu wa Efeso 4:6 inayosema" Kuna Mungu mmoja na Baba wa wote ambaye yuko juu ya wote ,anafanya kazi katika yote na yuko katika yote,amesema Baba Halisi alipokuwa akifafanua kuhusu sherehe hiyo na kuongeza wakati wa sherehe hiyo waumini wa kanisa hilo ,waalikwa na wananchi wote watatumia nafasi hiyo kuliombea Taifa na hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndio moyo mkuu wa Taifa la Tanzania."
Akifafanua zaidi kuhusu sherehe hizo ya kumletea Mungu Baba ambaye ndio Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake( Mathayo 21:43) ametoa mfano wa nchi za Magharibi wamekuwa na utamaduni wa sehemu ya 10 ya mapato yao na kutoa kwa Mataifa mengine."Tuje kwenye hii Sherehe au hiyo Ibada, nitoe mfano wa Magharibi wengi mnaweza kuwa hamfahamu ,Mataifa ya Magharibi unaweza kuona maendeleo waliyonayo lakini wanachagua Taifa moja ambalo wanaamini ni chanzo cha baraka, sehemu ya 10 ya mapato yao wanatoa hata kama hawamwambii mtu maana hiyo ndio kanuni ya maendeleo.
"Hata maji yakiwa yametuama halafu yakakosa sehemu ya kutolea lazima yataharibika, kwa hiyo hata weweazima sehemu 10 ya mapato yako uweke pale kwa hiyo Mataifa mengi yanafanya hivyo, inawezakana sisi hatufanyi lakini ndio kanuni ya maendeleo.Kwa hiyo tunapozungumza tutamletea aliyetuumba Matunda ya Shamba lake ni kanuni ya maendeleo."amesema kiongozi wa Kanisa hilo Baba Halisi .
Katika hatua nyingine amesema yeye kwa ufahamu alionao ameandika kitabu ambacho kinaelezea kuhuusu Taifa la Tanzania ambalo ni taifa lenye Baraka na kwamba mataifa ya magharibi walikuwa wanafahamu majira tuliyopita chanzo cha maendeleo kipo Mashariki ya Kati au Baraka chanzo cha Baraka kiko huku.“Kwa mujibu wa kitabu hiki utagundua chanzo cha Baraka kiko Tanzania sasa wengi wanawaweza wasikubali au wasiamini lakini kuna mbali ya kitabu kidogo kuna kitabu kikubwa nimeandika na mwezi ujao tutakizindua, kinazungumzia ufahamu ulionzia Tanzania kwenda mataifa mengine, kinathibitisha hiki ninachosema kwamba taifa hili ni chanzo cha Baraka.
“Kwa hiyo naomba msiwe mnaogopa kuandika habari za Kanisa Halisi la Mungu Baba ni za maendeleo na tumejikita katika kuhubiri amani, upendo usiobagua pamoja na uzalishaji, hibyo utaona tumejikita kujadili uchumi na maendeleo,”amesema Baba Halisi.
Ameongeza ndio maana hata kwenye Sherehe hiyo amealika watu wote bila kujali dini wala madhehebu yao kwa kuamini watu wote wameumbwa na mtu mmoja na ndio maana hata mvua inaponyesha haichagui bali inanyesha kwa wote kwasababu wote ni wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...