MKAZI wa Mwanza, Nickson Mfoi (20), amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kujitambulisha kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Mfoi ambaye ni mjasiliamali, amesomewa mashtaka yake leo Agosti 4,2022 na wakili wa serikali Ashura Mzava mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na Mzava imedai Septemba 22, mwaka 2021 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nia ya kulaghai umma mshtakiwa alijitambulisha kama Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika shtaka la pili inadaiwa, Oktoba 2, mwaka 2021, mshtakiwa alikutwa akitumia laini ya simu iliyokuwa ikimilikiwa na Getness Jackson bila kutoa taarifa kwa mtoa huduma.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na mdhamini mmoja muaminifu na mwenye kazi ambayo inaaminika akiwa na kitambulisho cha Taifa.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika, hivyo kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali( PH). Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 18, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...