Na. Damian Kunambi, Njombe

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Madini Steven Kiruswa imeunda timu ya wataalam itakayofanya kazi ya kuchambua leseni zote za miradi ya makaa ya mawe wilayani Ludewa mkoani Njombe zilizotolewa na kisha kutoa mapendekezo juu ya wachimbaji wadogo wakiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa pamoja na chama cha mapinduzi ili waweze kupewa maeneo ambayo hatatumia gharama kubwa ya uchimbaji.

Akiwasilisha taarifa hiyo katika kikao cha baraza la madiwani,Kampunga amesema kamati hiyo inahusisha MMI, NDC, mwanasheria wa Halmashauri, Afisa tarafa ya Mawengi pamoja na katibu wa mbunge ambayo imepewa majuma matano ya kushughulikia zoezi hilo na kutoa majibu.

Ameongeza kuwa kwa muda mrefu baraza hilo lilikuwa likitoa mapendekezo hayo ya ugawaji vitalu kwa wachimbaji wadogo kwakuwa maeneo hayo hayaja endelezwa kwa muda mrefu hivyo kwa hatua hiyo iliyofikiwa ni fursa ya kipekee ambayo inaenda kutimiza ndoto ya baraza hilo.

Aidha kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri Wise Mgina amempongeza mbunge kwa ufuatiliaji wake wa jambo hilo kwani endapo watagawiwa vitalu hivyo itasaidia kukuza uchumi wa Halmashauri na kuleta mzunguko mkubwa wa fedha kwa wilaya ya Ludewa.

"Halmashauri yetu ina miradi mingi ambayo ikifanyiwa kazi itakuza uchumi wetu, kila wakati baraza linapokutana tumekuwa tukiimba wimbo huu wa wachimbaji wadogo kupewa vitalu hivyo tunashukuru kwa walio tuwakilisha katika makubaliano hayo kwani mmefanya makubaliano yenye tija kwa halmashauri yetu", Amesema Mgina.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...