Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
MBUNGE Wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amewaasa wanaChalinze kujitokeza kuhesabiwa siku ya sensa bila kupuuzia na kuwaasa wale wenye ulemavu wa viungo mbalimbali wasiwafiche kwani kwa kufanya hivyo ni kuwakosea.
Ameeleza, imebakia siku moja hivyo wajiandae na kila mmoja anawajibu wa kumkumbusha mwenzie.
Ridhiwani ,akihamasisha wananchi wa Miono kushiriki zoezi la sensa ,alisema ni lala salama wasifanye ajizi ,kwani atakaekwamisha kuhesabiwa atakosea wenzie kupata takwimu sahihi ili kupata fursa ya maendeleo kwa usawa.
Ridhiwani ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi aliwataka pia watoe taarifa sahihi kujua wakulima wangapi,wafugaji, vijana ,wamachinga na makundi mengine ili hata kwa wakulima na wafugaji kujua takwimu sahihi ya mipango ya matumizi Bora ya ardhi ,ugawaji wa pembejeo na mengine.
"Nimefurahi utayari wa wananchi wetu kushiriki zoezi hili kwa ari kubwa sana,SensaKwaMaendeleo #KaaTayariKuhesabiwa"alisema Ridhiwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...