Raisa Said,Bumbuli
Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Tanga Husna Sekiboko amesema kuwa takwimu za sensa iliyopita Kwa Wilaya ya Lushoto haikulizisha Kutokana na wananchi Kushindwa kujitokeza Kwa wingi.
Hayo ameyasema Kata ya Vuga, Halmashauri ya Bumbuli wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuhamasisha wananchi kujitokeza Kwa wingi kuhesabiwa ifikapo agost 23.
Sekibo alisema kuwa sensa ya mwisho iliyofanyika mwaka 2002 wananchi wa Wilaya ya lushoto walishindwa kujitokeza kwa wingi kushiriki kuhesabiwa Kutokana na Imani potofu huku wakidai jambo hilo linakinzana na dini zote.
"Takwimu zilizoenda sensa iliyopita zilikuwa za uongo sababu nilishuhudia watu wengi walishindwa kushiriki kuhesabiwa kutokana na Imani potofu, sensa ya mwaka huu ni muhimu hivyo agosti 23 jitokezeni kuhesabiwa kwani sensa inatambuliwa na dini zote na sio kinyume kama mnavyosema" amesema huku akisisitiza wahakikishe wanatoa taarifa za kweli pindi Makarani watakapokuwa wanapita kuchukua taarifa zao..
Mbunge huyo alisema Sensa itawapeleka kwenye namba nzuri yakugawana keki ya Serikali,kipande hiki kiende wapi Kwa ukubwa upi na hata ili Mkoa uweze kugawanywa ni lazima idadi ya watu itambulike.
Alieleza kuwa lengo la sensa hiyo ni kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa.
Alisisitiza kuwa taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa
mgawanyo wa rasilimali.
Aidha ametoa mfano wa madhebu ya dini kwamba ili dhehebu lijenge nyumba ya kuabudia ikiwa ni msikiti au kanisa ni lazima viongozi wa dini wajue idadi ya waumuni wao
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wote watoe ushirikiano Kwa Makarani Watakao kuwa wanapita siku hiyo huku akisisitiza wahakikishe wanatoa taarifa za ukweli nakwamba taarifa hizo ni Siri.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa sensa sio jambo geni hasa Kwa wanawake kwakuwa wao Kila siku wamekuwa wakifanya sensa hata wanapofanya shughuli za nyumbani ikiwemo kununua chakula na mahitaji mengine.
Hata hivyo alisisitiza sensa inatambuliwa na dini zote sababu hata wao Kila siku wanapokutana kwenye jumuia ndogondogo huwa wanahesabiwa .
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Tanga Husna SekibokoMkuu wa Wilaya ya Lushoto Kaist Lazaro
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...