Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya burudani na michezo SportPesa, leo imetangaza rasmi kuingia mkataba na Klabu ya Singida Big Stars kama Mdhamini Mkuu kwa mara nyingine kuanzia msimu huu wa mwaka 2022/2023 mpaka msimu wa mwaka 2025/2026.
Hafla hiyo ya kumtambulisha mdhamini mkuu imefanyika kwenye ofisi za SportPesa, Oysterbay jijini Dar es Salaam. walioshiriki ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Sportpesa, Mh Tarimba Abbas, na kutoka Singida Big Stars ni Kanu Muhibu ambaye ni Mkurugenzi Uendeshaji Masoko na Fedha wa Klabu na baadhi ya wachezaji.
Akizungumza kwa niaba ya SportPesa Tarimba Abbas alianza kuelezea lengo la Sportpesa, ambayo ni kuona soka la Tanzania linapiga hatua na kwenda mbele kwenye ushindani wa juu zaidi kwa kuchangia kwenye kuendeleza mpira wa Tanzania na hivyo kusema udhamini wanaopatia Singida Big Stars ni kutimiza nia yao ya siku zote tangu wameanza biashara hapa nchini.
“Kama mtakumbuka tangu tumeanza biashara mwaka 2017 tulianza na dhamini za klabu pamoja na miradi mbali mbali ya kuinua soka la Tanzania. Hawa Singida Big Stars, zamani Singida United, tuliwadhamini wakati ule kwa mkataba wa Mwaka mmoja. Leo tunatangaza kuwadhamini tena, kwa mkataba wa miaka 4, kuanzia msimu huu wa ligi, unaoanza hivi karibuni”.
Akizungumza kwa upande wa Singida Big Stars, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Masoko na Fedha, Kanu Muhibu amewashukuru Sportpesa kwa kukubali kuwa wadhamini wao wakuu na pia kwa kuwa mstari wa mbele katika kukuza mpira wa miguu katika nyanja mbali mbali.
“Napenda kukukushukuru Mhe. Tarimba kwa kuwa bega kwa bega na timu za Tanzania na pia kuwashukuru SportPesa kwa namna mnavyojitoa kusaidia katika kukuza na kuendeleza mpira Tanzania. Leo ni siku ya kipekee kwetu kuweza kusaini mkataba huu na pia kumtambulisha mdhamini wetu SportPesa ambaye ametupa mkataba mrefu wa miaka minne’’. Alisema Muhibu.
Ameahidi kwamba watasimamia vipengele vyote kama vilivyoainishwa katika mkataba na kuhakikisha wanapata matokeo ambayo yatakuwa chachu ya kuendeleza biashara na mahusiano baina yao.
‘’Mimi kama kiongozi katika timu, pamoja na watendaji wengine wote wa Singida Big Stars ninaahidi tutatoa ushirikiano wa kutosha katika kutimiza, kufanikisha yale yote yaliyomo ndani ya mkataba huu. Kwa leo sina mengi sana zaidi ya kuwashukuru Sportpesa Pamoja na vyombo vya habari ambavyo vimekuwa nasi siku zote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...