Njombe
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah ametoa tahadhari na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuwa makini kutokana na vitendo vya utapeli vilivyoanza kutokea katika mkoa wa Njombe huku akibainisha kuwa mchungaji wa kanisa mojawapo mkoani humo ametapeliwa milioni 261 na watu wasiojulikana.
“Kumetokea utapeli na udanganyifu mkubwa unaoendelea hapa Njombe,ukitaka kununua kitu cha thamani hakikisha umejithibitishia kwanza kwa kuwa Njombe umeingia utapeli na utapeli huu unafanyika katika viunga vya madhehebu fulani na baadhi ya viongozi wa dini wamefanyiwa utapeli”amesema Kamnda Issah
Kamanda Issah amesema jeshi hilo linawashikilia watu mbali mbali wanaohusika na matukio ya utapeli huku akibainisha kuwa mchungaji wa kanisa mojawapo mkoani humo ametapeliwa kiasi cha shilingi Milioni 261 huku mtu mwingine wa kawaida akitapeliwa Milioni 75.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...