
Naibu Waziri Anthony Mavunde akipata Maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Taifa la Bima(NIC) Justine Iseni wakati alipotembelea banda la shirika hilo kwenye maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amesema kuwa katika kuhakikisha wananchi wanapata bima ya kilimo ni kazi sasa kwa shirika la Taifa la Bima (NIC) kuwafikia wakulima kupata bima hizo.
Mavunde aliyasema hayo wakati alipotembelea Banda la NIC katika Maonesho ya Kitaifa Kilimo Nane Nane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Amesema bima za kilimo ni muhimu sana kupata wakulima lakini wanahitaji elimu hiyo ili waweze kukata na sekta hiyo kuwa na uhakika pale majanga ya wakulima yanapowakuta.
Mavunde amesema kuwa sasa ni wakati mwafaka NICkwenda kwa wakulima wapate elimu ya bima kwani kilimo ni uti wa mgongo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...