Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PanAfrican Energy Tanzania, Andy
Hanna alipotembelea banda la kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa
kongamano la nishati Tanzania lililofanyika ukumbi wa JNICC jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Orca
Energy ambayo ni kampuni mama ya PanAfrican Energy, Jay Lyons wakati wa
kongamano la nishati Tanzania 2022 lililofanyika ukumbi wa JNICC jijini
Dar es Salaam.
PanAfrican Energy Tanzania (PAET) imetangaza kujivunia kuwa mdhamini wa Kongamano la Nne la Nishati Tanzania 2022. Hafla hii ya kila mwaka imefanyika chini ya uangalizi wa Wizara ya Nishati Tanzania, imekuja na kaulimbiu "Awamu Inayofuata katika Sekta ya Nishati Tanzania: Kukuza Uwekezaji na Ukuaji".
PAET ni mmoja kati ya wafadhili wawili wa platinamu kwa hafla ya mwaka huu. Pia, Orca Energy Group ambao ni kampuni mama ya PAET, imeratibu majadiliano ya jopo la mawaziri na kutoa wasilisho la kielimu kuhusu usimamizi wa hifadhi zilizokomaa.
Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa PAET, Andrew Hanna alisema, “Tunafuraha kubwa kuhusu kongamano hili litakaloleta mwelekeo kwenye sekta hii hapa nchini. Ni fursa nzuri ya kupata muda na wasimamizi pamoja na serikali, kubadilishana mawazo kuhusu sekta ya nishati na kile kinachohitajika ili kuhakikisha uhakika wa uzalishaji kwenda mbele, ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya gesi katika uchumi wa viwanda wenye mafanikio makubwa.”
Orca Energy Group, kampuni mama ya PAET, inaendelea kuwekeza katika shughuli zake za Songo Songo ili kuendana na ukuaji wa Tanzania katika uzalishaji wa umeme na upanuzi wa viwanda. Katika miaka miwili iliyopita, kampuni imewekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 70 katika kuongeza na kuendeleza usambazaji wa gesi, ikiwa ni pamoja na dola za Marekani milioni 42.5 katika mradi wa ukandamizaji wagesi katika kiwanda cha kuchakata gesi kinachomilikiwa na Songas ambacho kinaendeshwa n PAET, na zaidi ya dola za Marekani milioni 31.6 zilizowekezwa kukarabati visima vitatu. Pia hivi majuzi kampuni imetenga dola za Marekani milioni 20 kutekeleza uchunguzi wa ardi yenye eneo la takriban kilomita za mraba 200 katika eneo la Songo Songo mwishoni mwa 2022 ili kutoa taswira kamili ya changamoto zinazoweza kujitokeza katika eneo hili wakti wa utafutaji wa gesi na muelekeo wa rasilimali hiyo
PAET iliwakilishwa vyema kwenye Kongamano hilo na mameneja wakuu na takriban wafanyakazi wake wote wa Tanzania, wakati Orca pia iliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni, Jay Lyons, CFO wake, Lisa Mitchell, na wakurugenzi watendaji wawili wa bodi ya ORCA Energy, akiwemo Dk. Frannie Léautier na Linda Beal. Dk Léautier aliratibu mazungumzo ya "Kikao cha Mawaziri wa Kimataifa: Kuboresha Uchumi wa Afrika Kupitia Upanuzi wa Maendeleo ya Soko la Sekta ya Nishati". Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuangazia mtazamo wa nishati wa bara hili pamoja na uwezo wa Tanzania kama msambazaji mkuu wa nishati kimataifa.
Mhandisi wa PAET. Revocatus Kasheshi, pia alitoa mada maalum ya kielimu kuhusu usimamizi wa hifadhi zilizokomaa, kwa kutumia uzoefu wa miaka 18 iliyopatikana katika uzalishaji wa gesi Songo Songo.
PAET pia ilikuwa na banda la maonyesho kwa muda wote wa kongamano ili kuwapa wageni fursa ya kuzifahamu shughuli zinazohusu kampuni kama mzalishaji wa kwanza wa gesi nchini, na michango yake kwa uchumi wa Taifa - moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
Kongamano hilo lilifunguliwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na viongozi wengine wengi wa ndani na nje ya nchi huku wakijadili masuala yanayohusu kujenga uwezo wa ndani, ukuaji endelevu na muelekeo wa nishati safi pamoja na masuala mengine.
Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi ORCA Energy, Dkt. Frannie Leautier
akizungumza kwenye kongamano la Nishati Tanzania 2022 wakati wa mjadala
wa " Uboreshaji Uchumi wa Afrika Kupitia ya Sekta ya Nishati" Improving
Africa's Economic Through Energy Sector Market Development Expansion.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...