
Mtaalamu wa Sayansi ya chakula kutoka Idara ya Usalama wa Chakula kutoka Wizara ya Kilimo, Mercy Butta akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya katika maonesho ya Wakulima maarufu kama Nane Nane.
SERIKALI kupitia Mradi wa Kuzuia Sumu Kuvu wa 'Tanzania initiative for preventing aflatoxin contamination' (TANIPAC) ulio chini ya Wizara ya Kilimo wameendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuimarisha usalama wa chakula kwa wananchi na kuimarisha afya ya jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya katika maonesho ya Wakulima maarufu kama Nane Nane, Mtaalamu wa Sayansi ya chakula kutoka Idara ya Usalama wa Chakula kutoka Wizara ya Kilimo, Mercy Butta amesema kuwa mradi upo kwaajili ya kuimarisha biashara za mazao ya chakula ndani na nje ya nchi.
Kama tunavyofahamu Tanzania ni nchi kimbilio la chakula kwa mataifa mengi." Amesem Mercy
Amesema kuwa Mradi huo upo katika Halmashauri 18 ambazo ni Halmashauri ya Itirima, Buchosa, Bukombe, Kasulu, Kibondo, Urambo, Wilaya ya Nzega, Bahi, Kongwa, Chamba, Babati, Kiteto, Kilosa, Gairo, Nanyumbu, Namtumbo na Newara kwa upande wa Zanzibar ni Unguja na pemba.
Amesema wapo katika Maonesho ya Nane nane kutoa elimu kuhusu masuala ya sumu kuvu ili kila mwananchi apate elimu hiyo na aweze kuepuka kutokana na madhara yake.
Akielezea maana ya Sumu Kuvu Mercy amesema kuwa ni Sumu inayosababishwa na Fangasi kwenye mazao mbalimbali.
Tupo hapa kuwaeleimisha wananchi kuwa madhara ya Sumu Kuvu ni halisi, ukila chakula chenye Sumu Kuvu kwa muda mrefu unaweza kupata Kansa ya koo, Kansa ya Ini.
Amesema kuwa Maradhi ya Kansa yapo mengi kipindi hiki na asilimia 30 yanasababishwa na ulaji wa vyakula vyenye sumu kuvu.
Hata hivyo amesema sumu kuvu ni hatari kwani ikiingia kwenye mazao ni vigumu kutoka iwe kwa kupika au kukaanga hivyo wataendelea kutoa elimu kupitia mradi huo ili kuweza kumaliza tatizo hilo hapa nchini.
Amefafanua kuwa ili kuweza kudhibiti sumukuvu wakulima wanapaswa kufuata kanuni bora za kilimo ikiwemo kupanda kwa nafasi pamoja na kuvuna kwa wakati.
Pia amesema kunateknolojia ambazo wizara ya kilimo ikishirikiana na Kampuni ya Aflasafe na wadau wengine wa utafiti wamekuja na mbinu na teknolojia mbalimbali zinazoweza kudhibiti Sumu Kuvu.
"Tunayo Aflasafe ambacho ni kiwatilifu cha kibayolojia, ambacho hakina kemikali unatumia kiumbe hai kupambana kupambana na kiumbe hai mwingine.
Kwahiyo kwenye Aflasafe wamepandikizwa kuvu wa aina nyingine ambao wanapambana na kuvu ambao wanasababisha Sumu Kuvu." Amesema Mercy
Amesema kuwa Mkulima akitumia mbinu hiyo pale kabla mbelewele kutoka kwenye mazao yakiwa shambani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...