NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MBEYA
MAONESHO ya Nanenane Kitaifa 2022 yameanza rasmi ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameyazindua Agosti 1, 2022 kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Maonesho ya Nane Nane huwaleta pamoja Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Makampuni yanayojishughulisha na shughuli za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, Taasisi za Umma na Binafasi.

Miongoni mwa Taasisi zinazoshiriki kwenye Maonesho hayo ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF).

Akizungumzia ushiriki wa Mfuko kwenye Maonesho hayo, Meneja wa PSSSF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Ramadhani Mgaya amesema, Maonesho hayo ni jukwaa zuri kwa Mfuko kukutana na Wanachama na Wananchi kwa ujumla ili kutoa Elimu na kuwahudumia.

“Tunawakaribisha Wanachama wetu na Wananchi kwa ujumla kutembelea banda letu ili tuwahudumie, pia kupata Elimu kuhusu Mafao yatolewayo na Mfuko, Wastaafu Kuhakiki Taarifa zao, Wanachama Kupata Taarifa za Michango, na kutatua changamoto mbalimbali ambazo Mwanachama atakuwa nazo.” Alifafanua.

Alisema PSSSF imewekeza katika Maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kiwanda cha kuchakata Tangawizi cha Mamba Miamba, lakini pia Kiwanda cha nyama Nguru Ranch Hills LTD kilichoko Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro. "Uwekezaji huu unaakisi kauli mbiu ya Maonesho ya mwaka huu yasemayo “Ajenda 10/30 Kilimo ni Biashara; Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi". Alisema.

Aliwahakikishia Wanachama na Wananchi kuwa watakapofika kwenye banda la PSSSF watapatiwa huduma kama zinazopatikana kwenye ofisi za Mfuko zilizoenea nchi nzima Bara na Viasiwani.
Kikosi Kazi cha PSSSF kikiwa tayari kuwahudumia Wanachama na Wananchi wanaofika kwenye banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Nanenane viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Ramadhani Mgaya (kulia) akimuhudumia Mwanachama aliyetembelea Banda la Mfuko huo Agosti 2, 2022.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Ramadhani Mgaya (katikati) na Mwanachama wa PSSSF wakimsikiliza Afisa Uhusiano Mkuu PSSSF, Bi. Rehema Miamba kwenye Banda la Mfuko huo jijini Mbeya leo Agosti 2, 2022.
Alex Bwanakunu (kushoto), Afisa Huduma kwa Wateja PSSSF, akimuhudumia Mwanachama.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Ramadhani Mgaya (kushoto), akizungumza na Baltazar Mugori, Afisa Mafao Mwandamizi
Mwanachama wa PSSSF akiwa na kijitabu chenye taarifa za Mfuko wakati alipotembelea Banda la PSSSF kuhudumiwa.
Afisa Huduma kwa Wateja, Bi. Saluna Ally (kulia) akimuhudumia Mstaafu aliyefika kwenye Banda la Mfuko kuhudumiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...