Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Daniel Chongolo amesema kazi ya Serikali ni kutafuta njia ya kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo mbalimbali na sio vinginevyo na kwamba hategemei kuona Serikali ikikaa kimya wakati wananchi wanalalamika.
Amesisitiza Serikali kazi yake ni kuweka mipango ya kutatua changamoto husika na Serikali imethibitisha dhamira na jukumu lake la kutekeleza hilo kwani Wananchi
Chongolo ametoa kauli hiyo leo Agosti 2,2022 alipokuwa akizungumza na Wananchi na wanaCCM wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wakati akikagua mradi wa Ujenzi wa Kituo Cha afya kilichopo Kijiji cha Chekimaji.
"Niwapongeze kwa kupata kituo Cha afya kizuri sana na hongereni kwa kuletewa fedha nyingi lakini kubwa niwaletee salamu za Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wakati namuaga kumueleza nakuja Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kusalimiana na kuwatembelea Wana CCM na wananchi ameniambia awasilimu sana.
"Niwahakikishie anawapenda sana, changamoto zenu anazijua ikiwemo barabara ya TPC mpaka Boma kwa hiyo muwe na uhakika kwamba ataweka msuko na kuipa kipaumbele kuhakikisha inajengwa. Ndugu zangu nimewapongeza kwa kupata fedha za kituo cha afya lakini niwapongeze zaidi kwa ninyi wenyewe kuchanga zaidi ya Sh. milioni 11
"Kuhakikisha mnanzisha ujenzi wa zahanati kwasababu mlikuwa mnajua madhila ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma za afya, hongereni sana ,lakini niipongeze Halmashauri ya wilaya kwa kuona jitihada zenu na kuleta Sh.milioni 28 kuongeza nguvu zenu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo tulilosimama hapa la OPD ambalo fedha kwa ajili ya kituo cha afya zililikuta tayari limeshapauliwa, hongereni sana ,"amesema Chongolo.
Aidha amewapongeza kwasababu michango waliyotoa ilionesha dhamira yao ya kujikwamua na changamoto ya umbali wa kufuata huduma za afya a hiyo inoanesha ni namna gani walivyowazalendo na wanavyojipenda kujitafutia kwa kutumia nguvu zao na namna ya kusogeza huduma karibu yao.
"Lakini niipongeze Serikali baada ya kuona jitihada zenu kwa kuanza na halmashauri kwa kuwaongezea nguvu na fedha Sh.milioni 28 lakini Serikali Kuu ikaleta milioni 250 mara mbili na kuongeza milioni 90 juu yake , hongereni sana Serikali
"Kazi ya Serikali ni kutafuta njia ya kutatua changamoto za wananchi na sio vinginevyo hatutegemei kuona Serikali ikipiga porojo hatutegemei kuona Serikali ikipiga nne wakati wananchi wanapata shida , wananchi mkilia shida fulani , Serikali kazi yake ni kuweka mipango ya kutatua changamoto husika.
"Na hapa Serikali imethibitisha dhamira na jukumu lake la kutekeleza hilo kwani Wananchi walionesha dhamira ya uhitaji wakatenga eneo wakaanzisha michango ya kwao,wakaweka mazingira Serikali ikasema naam kwasababu mnauhitaji ikaleta Sh.milioni 250 za kwa kwanza ,ikaleta milioni 250 za pili na ikaleta Sasa milioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi.
"Hiyo ndio kazi lakini wakati kazi inaendelea na watumishi wa afya wameshafika hapa , hongereni sana Serikali , moja ya changamoto kubwa ya sisi ni kulaumu , tunasubiria mambo mabaya tu yatokee tubakie tunalaamu pale wanapofanya kazi nzuri watumishi wa Serikali na watendaji wa Serikali hatupongezi,"amesema Chongolo
Amefafanua pale Serikali inapofanya jambo jema la utekelezaji wa Ilani ambayo wamewapatia kutekeleza kwa kipindi cha miaka mitano wananchi hawafanyi chochote cha kuwapongeza hivyo ni lazima jamii ijenge utamaduni wa kupongezana pale wanapofanya mambo mazuri au wengine wanapofanya mambo mazuri.
"Tusisubiri kulaumu na kutenengeneaza nongwa kwasababu binadamu ana pande zote mbili, kukosea ni sehemu ya maisha lakini kupatia pia si lazima tuwape mkono hongereni sana watumishi wa Serikali kwa kufanikisha hili , mmesema hapa barabara na mimi niwahakikishie barabara hii itajengwa.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM,) Daniel Chongolo akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya na nyumba ya watumishi katika Kata ya Masama Rundugai Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.Pichani kulia ni Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe.Saashisha Mafuwe
Katibu Mkuu wa Chama cha Mainduzi (CCM,) Daniel Chongolo akisikiliza taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt. Itikija Msuya mara baada ta kukagua mradi huo
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akikagua majengo ya
kituo cha afya ya Kata ya Masama, Hai Mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akikabidhiwa fimbo ya kimasai baada ya kuvalishwa vazi la kimila alipofika kukagua mradi huo wa kituo cha Afya ambao utasaidia upatikanaji wa huduma za Afya kijijini hapo.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na baadhi ya akina Mama baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya na Nyumba za Watumishi katika kata ya Masama Rundugai kijiji cha Chekimaji wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe.Saashisha Mafuwe akizungumza jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM ,Daniel Chongolo mara baada ya kukagua majengo ya kituo cha afya ya Kata ya Masama, Hai Mkoani Kilimanjaro.Katibu MKuu wa CCM Daniel Chongolo na Ujumbe wake wakifurahia jambo
Wakaazi wa eneo la Masama wakifurahi jambo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...