Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MKUU
wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amekutana na uongozi wa Shirika la
Maendelo la Taifa - NDC kwa mazungumzo ya kuitangaza Kongani ya Viwanda
inayomilikiwa na Shirika hilo ,Mjini Kibaha na kuhakikisha inaandaa
mchoro wa eneo hilo kwa ajili wawekezaji.
Mazungumzo
hayo yalifanyika kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa huo ambapo Kunenge
amemshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Nicolaus Shombe
kuhakikisha ofisi yake inaandaa mchoro huo ili kuinua uwekezaji.
“Ni
wajibu wangu kuzisemea taasisi zote zilizopo mkoani kwangu, hivyo
mnapaswa kuandaa mchoro wa eneo hilo, mnipatie ili tuweze kulitangaza
kwa wawekezaji wanaotafuta maeneo ya uwekezaji,” alisema Kunenge.
Akifafanua
faida za uwekezaji, Kunenge ameeleza kuwa unasaidia katika kufanisha
malengo ya mkakati mkubwa wa mkoa wa kuongeza vyanzo vya mapato, hivyo
eneo hilo la NDC ni muhimu na litasaidia kuongeza mapato.
Katika
Hatua nyingine, amewapongeza watendaji wote wa Sekretarieti ya Mkoa na
wa Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kwa utendaji wa kazi na kupelekea
mkoa kushika nafasi ya tatu nchini kwa kigezo cha makusanyo yanayotokana
na mapato ya ndani.
Pia Mkurugenzi Mtendaji Wa shirika la Maendeleo ya Taifa NDC Dr. Nicolaus
Shombe alifafanua kuwa Kongane la Viwanda TAMCO, Kibaha lina eneo ukubwa
wa ekari 201.63 na limeteuliwa kujenga Viwanda katika Makundi matatu
aliyoyataja kuwa ni Viwanda vya madawa na vifaa tiba, viwanda vya
kuunganisha magari na mitambo pamoja na viwanda vya nguo.
Alisema eneo hilo linahitaji miundombinu ya barabara kama kilomita 4.8 na tayari Kilomita 1.6 imeshajengwa.
Dr.
Shombe alieleza ,tayari eneo hilo limepelekewa umeme wa Kv 33 na
TANESCO huku miundombinu ya maji ikiwa inaendelea kuboreshwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...