Dkt. Biteko ametoa
pongezi hizo baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha mkaa mbadala wa
kupikia unaojulikana kama Rafiki Coal Briquettes unaotokana na makaa ya
mawe kilichopo jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Biteko amesema, pamoja na Serikali kuendeleza juhudi za kupambana na
matumizi ya mkaa utokanao na misitu na badala yake kutumia nishati
mbadala, STAMICO imeunga mkono jitihada hizo kwa kuanzisha kiwanda cha
kuzalisha mkaa wa mawe kwa ajili ya matumizi ya kupikia majumbani.
Aidha,
Dkt. Biteko amesema kwa sasa STAMICO ina jumla ya uwekezaji wa zaidi ya
kiasi cha shilingi bilioni 63.1 ukilinganisha na miaka michache
iliyopita ambapo Shirika lilifisika na kutaka kufungwa.
Pia,
Dkt. Biteko amesema STAMICO imeagiza mitambo mipya 11 kwa ajili ya
uchorongaji na mitambo 4 kwa ajili ya kuzalisha makaa ya mawe ili
kuongeza uzalishaji wa makaa hayo na kukidhi mahitaji ya watanzania
ambapo mitambo hiyo itasimikwa jijini Dodoma, Songwe, Pwani na Kanda ya
Ziwa.
Naye, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amesema, Shirika hilo
lina mkakati wa kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji wa kutosha ili
kukidhi mahitaji ya watanzania ambapo limeagiza mitambo miwili yenye
uwezo wa kuzalisha tani 20 za makaa hayo kwa saa.
Dkt.
Mwasse amesema, mradi huo unatarajia kuwanufaisha watanzania kwa kutoa
ajira na utapunguza janga la ukataji miti kwa ajili ya mkaa hivyo
kuchangia kutunza mazingira.
Dkt.
Mwasse amesema STAMICO imeanza kusambaza nishati hiyo ambayo ni nafuu
zaidi na rafiki kwa mazingira baada ya kuidhinishwa na Shirika la
Viwango la Taifa (TBS) tayari kwa matumizi baada ya uzalishaji wa
majaribio kufanyika kwa ufanisi.
Aidha,
Dkt. Mwasse amesema mkaa huo una faida lukuki na baadhi amezitaja kuwa
ni pamoja na rafiki wa mazingira, kuokoa pesa nyingi zinazotumika kwenye
nishati nyingine, mkaa wa mawe wakupikia unadumu jikoni kwa muda mrefu
kuliko mkaa wa miti hivyo kuzidi kupunguza gharama za matumizi ya
nishati hiyo, huboresha usafi wa jikoni na maeneo ya nyumbani
yanayochafuliwa na mkaa wa miti.
Pamoja
na mambo mengine, Dkt. Mwasse amesema, misitu ni muhimu kwa maisha ya
binadamu na viumbe hai kwa kuwa huifadhi vyanzo vya maji, kuboresha hali
ya hewa, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, malisho ya mifugo, kuboresha
shughuli za kilimo na kuboresha mandhari ya nchi mijini na vijijini
ambapo amewataka watanzania kuunga mkono matumizi ya makaa hayo ambayo
matumizi yake ni rahisi na hupika kwa haraka zaidi na yana faida nyingi
kuliko mkaa wa miti ambao athari zake kimazingira ni kubwa.
Dkt.
ameongeza kuwa, kutokana na manufaa ya mkaa huo, tayari STAMICO
inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa jamii kubwa inanufaika na
inatumia mkaa huo ambao ni wazi utasaidia kufanikisha kampeni ya
utunzaji wa misitu ambapo kwa kuzingatia umuhimu wake, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isidor Mpango anatarajiwa
kuuzindua rasmi mkaa huo Agost 12, 2022 ili uanze kutumika rasmi na
watanzania wote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...